Hilo neno NFT kwa dunia ya sasa hivi sio geni sana, pengine inawezekana ushawahi kulisikia au kupishana nalo sana huko mtandaoni.
Hapa kuna maswali ya kujiuliza je NFT zina thamani ya hela kweli au ni maneno tuu na mambo ya kukuza kupitia katika mtandao?

NFT ni kitu gani sasa? Hilo ndio swali kubwa hapa sio?
Kwa haraka haraka ni kwamba NFT ni mali ya kidijitali (Digital Asset) ambazo huwa ziko katika mfumo wa vitu vya kawaida kabisa kama vile muziki, vitu ambavyo viko ndani ya magemu (in-game), video na aina zingine za Sanaa.
Vitu hivi vinanunuliwa katika mtandao (online) na mara kwa mara vinanunuliwa na pesa ya mtandao (Crypto Currency) na huwa zinakua na mfumo wake wa programu unafanana na wa Crypto unaojulikana.
Teknolojia hii imeanza kupata jina sana mwaka 2014, na ukiachna na hilo ni kwamba kila siku NFT zinazidi kuwa maarufu tuu.
Imekau ni njia ya kawaida sana kwa dunia ya sasa ya kuwwezesha kununua na kuuza Sanaa ya kidijitali (Digital Art).
Soko la NFT lilionekana kukua sana kwani kwa mwaka 2021 tuu soko lake lilikua na thamani ya dola bilioni 41 za kimarekani.

NFT ni moja kati ya vile vitu amabavyo viko vya kipekee na mtu haweza akatengeneza kopi yake na havina mbadala mfano mzuri ni picha maarufu ya monalisa n.k.
Hii inamaanisha ukiwa na NFT ya aina Fulani ni wewe tuu ambayo utakau nayo wewe tuu. Ni wazi vitu kama hivi lazima viwe na thamani ya juu.
Kwa ufupi hio nadhani iutakua ushaelewa ni nini maana ya NFT.
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Sarafu Ya Kidigitali >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini hili umelipokejae hili? Je uko tayari kumili mali za kidigitali kwa mfumo huu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.