fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

NASA Waja na teknolojia mpya ya WiFi – Kutumia Chaji Kiasi Kidogo Zaidi

NASA Waja na teknolojia mpya ya WiFi – Kutumia Chaji Kiasi Kidogo Zaidi

Spread the love

Ni wazi kwamba tupo katika kipindi cha ushindani katika uvumbuzi wa teknolojia hasa za mawasiliano, teknolojia nyingi zimekuwa zikiibuliwa na wanasayansi na watafiti kwa kasi kubwa. NASA wamekuja na teknolojia mpya ya WiFi ambayo itapunguza maradufu matumizi ya umeme (betri), uvumbuzi huu unategemewa kuleta mbadiriko makubwa katika ubunifu wa vifaa vya mawasiliano vinavyotumia WiFi.

wifi-nasa-teknolojia

Teknolojia hii ya NASA itafanya kiasi cha chaji kutumika kiwe kidogo sana kwa zaidi ya mara 1000 ya matumizi ya chaji kwa teknolojia ya sasa ya WiFi.

Katika mfumo wa WiFi tunaotumia sasa ni kwamba kifaa chako kinatengeneza mawimbi na kuyaongeza nguvu kisha huyatuma mawimbi hayo kuielekea ruta yako, shughuli hii nzima ya kutengeneza mawimbi na kuyakuza kisha kuyatuma ndiyo hasa inayotumia nguvu nyingi kotoka katika betri ya kifaa chako.

329811-wifi

Teknolojia ya WiFi ni moja ya teknolojia muhimu sana katika matumizi ya kila siku ya vifaa vya elektroniki kama vile simu janja, tabelti na kompyuta

NASA ni shirika la kimarekani linalojihusisha na masuala ya usayansi wa sayari yetu na zinginezo, na ili kufanikisha tafiti zao wanajikuta katika juhudi kubwa za kufanya ugunduzi wa teknolojia za kisasa kwa ajili ya kurahisisha tafiti zao na pia utengenezaji wa vifaa vyao vinavyosafiri nje ya dunia.

Adrian Tang ambaye ni mtafiti katika katika maabara za NASA pamoja na profesa M.C. Frank Chang kutoka katika chuo cha California Marekani wametengeneza chip ya WiFi ambayo badala ya kutengeneza mawimbi yake kwenda katika ruta yenyewe huongeza data katika mawimbi yanayotoka katika ruta na kisha huyaakisi mawimbi hayo kurudi katika ruta.

 Soma Pia“Wi-Gig” Teknolojia Inayofuata Baada ya “Wi-Fi”

Huu ni mwendelezo wa tafiti mbali mbali ambazo zinalengo la kuboresha huduma za mtandao za wireless, siku kadhaa zilizopita tuliandika kuhuu teknolojia ya WiGig ambayo pia ni mmoja ya jitihada za kutaka kuboresha mfumo huu wa WiFi. Ni jambo zuri kuona watafiti wanazidi kujitaidi kuboresha ukaaji wa muda mrefu wa vifaa vyetu bila kuchaji chaji kila saa.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania