fbpx

Udukuzi wa taarifa za wateja unatesa mabenki

0

Sambaza

Data za wateja wa benki kuu ya Thailand (BOT) zimedukuliwa katika matawi mawili makubwa ya kibiashara na wadukuzi ambao hawajajulikana mpaka sasa.

Kulingana na shirika la habari la Sinhua, benki za ‘Kasikorn bank’ na ‘Krung Thai Bank’ zimethibitisha kuwa data za wateja zaidi ya 120 elfu zimeibiwa.

Wakati wataalam wa usalama wa mitandaoni kutoka benki kuu ya Thailand (BOT) wameahidi kuongeza hatua ulinzi wa taarifa za watu mitandaoni, watendaji wa benki zilizoathiriwa na udukuzi wamedai kuwa hawakuona dalili zozote za wizi wakati data hizo zikidukuliwa.

taarifa za wateja

Kwenye benki ya Krung mteja anyeomba mkopo kwa njia ya mtandao anatakiwa atume nakala ya kitambulisho chake, ameandikshwa takwimu za idadi ya watu, kipato chake na taarifa za matumizi yake kila mwezi kutoka benki.

Wezi hao wametumia mbinu za kisasa kupata taarifa za wateja zaidi ya mia moja na ishirini elfu kisha kutumia taarifa hizo kuomba mikopo kupitia mtandao.

taarifa za wateja

Wahusika wa benki hizo wote wamesema ingawa udukuzi wa taarifa za watu ulitokea lakini hakuna hata muamala uliofanyika ambao ni wa kutatanisha.

Ukuaji wa teknolojia umerahisisha sana maisha ya watu lakini changamoto yake kubwa ni udukuzi kutoka kwa makundi mbalimbali ya wasio waaminifu.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uchina: App kukutaarifu watu wenye madeni ya mikopo benki wakiwa karibu yako
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.