Kuna tetesi kwamba katazo la kutoingia na Laptop pamoja na Tablet katika ndege zinazofanya kati ya Marekani na nchi nane za kiisilamu linatokana kuwepo kwa taarifa juu ya magaidi kufanikiwa kutengeneza mabomu yanayofichwa katika vifaa hivyo bila kugundulika kirahisi.
CNN imeripoti kwamba kuna tetesi kwamba vyombo vya usalaama vya Marekani vimegundua kwamba magaidi wameweza kufanikiwa kutengeneza teknolojia ya mabomu ambayo yanaweza kuwekwa ndani ya Laptop bila kuathiri ufanyaji kazi wa kifaa hiki.
Kwa mujibu wa CNN ugunduzi wa taarifa hiyo ndio hasa ulikuwa chanzo cha Marekani kuzuia abiria wanaosafiri kutoka katika baadhi ya nchi, tetesi hizi zimepokelewa kwa hisia tofauti kwa Wamarekani na wapo ambao wanajiuliza kama katazo kwa viwanja kumi tu vya ndege litatosha kuepusha madhara yanayoweza tokana na shambulio kama hilo.
Tetesi hizi zinamaanisha nini?
Katika lugha nyepesi ni kwamba magaidi wameboresha teknolojia yao na sasa wanaweza kuficha bomu ndani ya laptop ama kifaa kikubwa cha electroniki bila kudhuru ufanyaji kazi wa kifaa hicho, teknolojia hii inawaruhusu magaidi kuweza kupenyeza mabomu katika ndege bila kugundulika.

Katazo hili linazihusu ndege zinazosafiri kwenda moja kwa moja nchini Marekani na wasafiri wanaweza kuweka laptop katika mizigo isiyoingia katika cabin ya ndege, na tayari baadhi ya mashirika ya ndege yameamua kuwaazima wasafiri waliokumbwa na kadhia hiyo Laptops ambazo watazitumia wakiwa katika safari hizo.