Pakistan imetoa amri kwa makampuni yanayotoa huduma za kisimu katika nchi hiyo kusitisha wateja kutumia huduma ya BlackBerry Enterprise mpaka kufikia november 30. Amri hii imetoka moja kwa moja toka mamlaka ya mawasiliano ya Pakistan ambayo wanadai usitisho huo ni kwa sababu tishio katika swala zima la usalama
BlackBerry Enterprise Services (BES) inaruhusu watumiaji wa simu za Blackberry kuweza kutengeneza njia za mawasiliano ambazo ni za siri, kuzifanya barua pepe na hata meseji za kawaida kuwa za siri na taarifa hizo kuhifadhiwa katika ‘eneo maalum la kuhifadhi data katika blackberry’. Hii inamaanisha kama njia hizi za mawasiliano zitaanzishwa basi hata serikali haitaweza ingilia na kujua nini kimetokea katika mawasiliano hayo.
“Kulikua na changamoto kutokana na kwamba huduma ya barua pepe katika blackberry haikuweza kufuatiliwa (track) au hata kuondoa usiri (Decode) ujumbe unaotumwa. Hii ni kinyume na usalama” – Amesema muongeaji wa PTA, Khurram Mehran
Kupigwa marufuku kwa huduma ya Blackberry Enterprise hakutahusisha kupigwa marufuku kwa huduma zingine kama vile BBM na Blackberry internet service (BIS). Hata hivyo kupigwa marufuku huku kwa huduma hii hakutakuwa na hasara kubwa kwa watumiaji kwani kuna watumiaji 5,000 tuu nchini Pakistan wanaotumia huduma hiyo ya BES
Serikali ya pakistan mara ya kwanza iliyaomba makampuni matatu makubwa ya simu – Mobilisk, Ufone na Telenor Pakistan – kuitaarifu (serikali) endapo watumiaji wake watatumia mawasiliano ya kisiri. Watoaji wa huduma za simu kwa sasa nchini humu wanatarajiwa kutoa notisi kwa watumiaji wa simu za blackberry na haswa wale wa huduma ya BES kuwa huduma hiyo itasitishwa/fungwa.
Hii sio mara ya kwanza kwa seriakali kupiga marufuku huduma fulani ya blackberry mfano India, Saudi Arabia na Indonesia, nchi hizi zote zilishawahi kutishia kupiga marufuku baadhi ya huduma za blackberry. Blackbeery nao pia hapo zamani waliweza kusitisha ‘kupigwa marufuku’ kwa baadhi ya huduma zake mara baada ya kuongea na serikali.
Zoezi hili ni la kimaendeleo lakini je wewe mwana teknolojia unalichukuliaje swala hili. tuandikie sehemu ya comment hapo chini. Pia usichoke kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom kwa masuala yote yanyohusu Teknolojia.
PTA = Pakistan Telecommunication Authority
No Comment! Be the first one.