Betri ya simu kuisha chaji haraka limekuwa tatizo kubwa kwa watumiaji wa simujanja, maana apps ni nyingi na matumizi ni mengi. Kwa sasa imewalazimu watu kuwa na powerbank au kununua simu ya ziada, lakini je kuna namna ya kuboresha na kufanya betri la simu lisiishe chaji haraka? Tujifunze.
Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vitasaidia kulinda Battery ya simujanja (smartphone) yako isiishe haraka.
1: Teknolojia ya kuruhusu mwanga ( Always on Dispaly ( AoD) & Widget)
Kipengele (Feature) cha Always-on-Display, hapa simu yako iko ON ikitumia mwanga zaidi kwa muda wote na hii huchukua wastani wa takribani 8% ya matumizi ya betri(Battery Life) kwa siku kwa simu janja ya kisasa. Kama iko ON, ikiwa unaangalia jumbe/notifications mara kwa mara, unaweza kuiweka OFF na ukawa unaifungua/unlock simu yako mwenyewe kuangalia notifications, pia weka Auto-Brightness option yaani simu yako iwe na uwezo wa kujipunguza na kujiongeza mwanga yenyewe.
2. Muda wa Kioo kupoteza Mwanga (Screen time out & WiFi/Mobile Data).
Mpangilio (Setting) ya Kioo/display yako isipoteze/zima mwanga kwa haraka (Phone Screen always ON) ina mchango mkubwa pia kwenye ulaji wa chaji kutoka kwenye betri lako. Pia uamuzi wa kuzima data/intaneti muda ambao hauitumii sana ni uamuzi pia utakaoongeza uwezo wa betri kudumu na chaji muda mrefu zaidi. Hii ni kwa sababu programu/apps ambazo zinafanya kazi bila ya wewe kujua (background apps) zinatumia intaneti/data ata pale ambapo hauitumii simu yako na husababisha betri kuisha haraka.
Vioo/Display za kisasa, mfano zile zinazotumika kwenye simu za Samsung – Super AMOLED zinahitaji umeme mwingi ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi, hiyo kama unatumia mpangilio wa kuruhusu simu kuendelea kuwa na mwanga ata pale ambapo haitumiki basi jua inatumia chaji nyingi zaidi.
Ushauri:
- Kufanya mabadiliko eneo hili kwa watumiaji wa Android nenda eneo la settings/mipangilio, alafu nenda Display, kisha Screen timeout. Hakikisha muda usizidi sekunde 30.
- Pia kama kuna muda hautatumia sana apps za kuhitaji intaneti basi hakikisha unazima Data/WiFi.
3. Kupunguza kiwango cha ubora wa teknolojia ya Display pamoja na manjonjo mengineyo ya urembo (Display settings & Motion Smoothness)
Kama unatumia simu bora za matoleo juu (Flagship Smartphones) hasa Samsung, iPhone, Google Pixel, OnePlus, Huawei, Xiaomi, Oppo n.k, unaweza kupunguza mipangilio ya ubora wa muonekano (Screen Resolution). Mfano kiwango cha ubora wa display/screen cha QHD Resolution kinatumia umeme mwingi kuliko Full HD, dispaly ikiwa QHD itahitaji uwezo mkubwa wa ufanisi (extra processing power) kuweza kufanya kazi kwa usahihi.
Ushauri:
- Unaweza kubadili Resolution kwenye Display settings, pia unaweza kutumia mpangilio wa Adaptive Brightness ambao utakusaidia wenyewe kubadili kiwango cha mwanga cha simu yako ili kufanya chaji idumu muda mrefu zaidi.
- Tumia mpangilio Mweusi, yaani Dark Mode. Kwani mpangilio huu pia unasaidia kupunguza utumiaji chaji kwa kiwango flani.
4. Kuzimwa kwa Apps zisizotumika (Sleep Mode for Apps)
Simu janja za Android (Android smartphones) kwa sasa zinafanya vizuri kwenye kutunza Memory (Memory management) pamoja na uwezo wa kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja (Multitasking), maboresho yote haya yamekuja pia na uwezo wa kuzuia Apps zinazofanya kazi nyuma ya pazia pale ambapo hauzitumii. Mpangalio unaofahamika kama “Background usage Limit” unasaidia sana kupunguza matumizi ya chaji ya apps ambazo hauna mpango wa kuzitumia hivi karibuni.
- Kwenye simu za Samsung na nyingine kuna mpangilio/Option ya “Put Unused Apps to Sleep” ambayo ukiweka inasaidia kuzuia Programu/Apps ambazo hutumii kwa muda huo kuwekwa kwenye sifa ya kulala (Sleeping Mode), yaani zinazuiliwa kufanya kazi ili kusaidia kupunguza matumizi yake ya chaji.
- Apps za mitandao ya kijamii kama TikTok na Instagram zinatumia kiwango kikubwa cha data/intaneti ambacho kinapelekea pia matumizi makubwa ya chaji, unaweza kuzuia baadhi ya vipengele/features kwenye apps hizo. Unaweza kuzuia video zisicheze bila kuruhusu (ukienda kwenye mipangilio chagua OFF kwenye ‘Auto Play’) kwenye Apps hizo ili kupunguza matumizi ya chaji.
5. Ondoa Apps Usizozitumia
Kuzima taarifa/Notifications kutoka apps ambazo huzitumii mara kwa mara pekee haitoshi, tunakushauri pia upitie apps zilizopo kwenye simu yako na kuziondoa zile ambazo hauzitumii (Uninstall). Pia kuna apps nyingi zinakuja na simu (native Apps/pre-installed apps) ambazo huwezi kuzitoa kwenye simu yako lakini ata kama hauzitumii bado zinafanya kazi na kutuma notifications mara kwa mara. Kwa apps hizi unaweza kuzizima ( “disable” au “Force Stop”) na unaweza kuzima uwezo wake wa kutumia intaneti/date (Ukienda kwenye mipangilio ya apps, kisha bofya “App Info” >> “Mobile data”).
Kama huwezi kuona apps zinazofanya kazi ata pale ambapo hauzitumi, yaani ‘running background Apps’ kwenye simu ya Android inabidi kuruhusu/enable Developer option (kiwango cha juu ya kuona mipangilio ya simu janja yako).
- Nenda kwenye Settings >> About phone >> Build Number “Bofya kwenye Build number mara 7“
- Baada ya hapo nenda kwenye developer option bofya kwenye “Running services”
- Hapo utafahamu apps/huduma ambazo huzihitaji ila zinafanya kazi ata pale ambapo haujazifungua
6. Boresha/Update Programu/Apps pamoja na mfumo wa simu (Software System)
Kutumia programu za simu zilizoboreshwa (updated Apps and latest Software system) inafanya utendaji kazi wa simu kuwa mzuri na hivyo kupunguza matumizi makubwa ya betri.
Unaweza kuangalia mfumo wa masasisho ya simu yako (System update) kwa kwenda kwenye Settings >> About phone >> System updates. Kama utaona kuna maboresho fanya maboresho/updates.
USHAURI
• Tumia chaja halisi na sahihi kwa ajili ya kifaa chako (original) kila mara unapochaji simu yako.
• Epuka kutumia simu ikiwa unaichaji, hii inaweza kusababisha kifaa chako kuongezeka kiwango cha joto. Betri linadumu vizuri kama halipati hali ya joto kali mara kwa mara.
• Usiruhusu simu yako iishe kabisa chaji (0%) ndipo uichaji.
• Usiweke simu sehemu yanye joto kali kwa muda mrefu au epuka simu yako kuchemka kwa muda mrefu kutokana na matumizi yaliyopitiliza.
No Comment! Be the first one.