Bidhaa za kidijiti kwa wale ambao tunapenda kuagiza vitu nje kwa bei ya ughaibuni tumekuwa tukitembelea masoko mbalimbali tukitafuta unafuu wa bidhaa husika lakini daima inatupasa kuvumilia kwa siku, wiki kadhaa au hata mwezi kuweza kuweka mikononi mwetu kile ambacho umekinunu kupitia tovuti fulani.
Sio jambo geni kusikia simu fulani inapatikana kwenye duka fulani linalomilikiwa na kampuni inayotoa huduma za mawasiliano nchini Tanzania. Ni ukweli usiopingika kuwa simu za Infinix zimepenya soko barani Afrika na hata kwa kampuni kama Vodacom Plc kuweza kurahisisha upatikanaji wa Infinix Zero 6.
Infinix Zero 6 ina sifa gani?
Kwa uchache tuu Infinix Zero 6 imewekwa nguvu nyingi sana kwenye upande wa kamera ambapo kamera za nyuma zina MP 12+MP 24 kuweza kupiga picha/picha jongefu zenye mng’ao wa hali ya juu sana nakamera ya mbele ina MP 20; mbali na kutoa picha nzuri pia ina teknolojia ya AI. Mbali na hapo kioo cha mbele kimewekewa ulinzi kioo cha Gorilla inchi 6.2. Uwezo wake wa betri ni 3650mAh pamoja na XCharge kwa ajili ya teknolojia ya kuchaji haraka.

Ilichokifanya Vodacom Plc na Infinix Mobile
Kwenye maduka ya Vidacom watu wataweza kununua simu hiyo ambapo Vodacom itakuwa ikitoa GB 4 kila mwezi (kwa muda wa miezi mitatu=GB 12) kwa wateja wenye rununu husika mbali na hapo pia wateja watapata zawadi nyingine kutoka dukani hapo.