Umewahi kujiuliza ni kwanini huwezi kutoa betri kwenye simujanja za kisasa kwa urahisi?
Kampuni za simu walianza kuleta simu ambazo mtumiaji wa kawaida hawezi zitoa kwa urahisi (non removable) kutokana na sababu mbalimbali. Leo tuzielezea zile muhimu.
Simu nyingi zamani zilitengenezezwa katika namna ilikuwa rahisi sana kuchomoa betri na kulibadilisha, lakini siku hizi kufanya hivyo kutakulazima uipeleke kwa fundi.
1: Kuzuia maji kuingia kwenye simu kwa urahisi.
Miaka ya nyuma ilikuwa changamoto kutengeneza simu zenye kuhimili uwepo wa maji (Water Proof) mpaka walivyogundua kuwa simu ambazo haziwezi kutolewa battery ni rahisi kutengenezea tabaka (layer) ili kuzuia maji yasiingie ndani ya simu kwa urahisi.
2: Usalama wa simu.
Simu ambazo haziwezi kutolewa betri kwa urahisi (Non removable battery) ni rahisi kuifatilia (track) endapo simu imepotea kwa sababu mwizi hawezi kutoa betri kwa urahisi hivyo ni ngumu kwa mwizi kuzima vipengele vya ulinzi kwenye simu (disabled security features).
3: Kuboresha mwonekano wa simu.
Simu ambazo unaweza kutoa betri kwa urahisi (removable battery) hazina muonekano mzuri kutokana na kuwepo kwa cover la juu ambalo hulinda battery ya simu ukilinganisha na simujanja za kisasa ambazo zina mwonekano mzuri sababu ya uwepo wa battery nyembamba ambayo pia huwezi kuitoa kwa urahisi.
Makala nzuri sana, hakika nimeelimika vya kutosha