Je simu na tableti zetu ni sawa ziwe na muonekano ule ule tuu mara zote? Itakuwaje kama simu yako utaiweza kuikunja kunja na kubadili umbo lake lakini kila kitu kikaendelea kufanya kazi kama kawaida?
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Bristol cha huko Uingereza wamekuja na teknolojia ambayo siku moja itaweza kufanya vitu ambavyo nimevielezea hapo juu kuweza kufanyika.
Teknolojia hiyo imehusisha utengenezaji wa vifaa vidogo vya umbo la boksi dogo ambapo pande zote zinaweza kuwa na kioo (display) na vinaweza kuunganishwa vingi kwa pamoja na vikafanya kazi kwa ushirikiano kama vile kifaa kimoja cha elektroniki.
Hii inamaanisha kama kifaa cha elektroniki kitaweza kutengenezwa kwa kutumia mjumuisho wa cubimorph kadhaa basi mtumiaji atakuwa na uwezo wa kubadilisha muonekano wa kifaa chake kama vile simu kwenda kwenye umbo alipendalo.
Changamoto?
Teknolojia hiyo inaweza kuja kuwa na changamoto zake pale ambapo mteja atataka kununua kitu fulani halafu baada ya kufanya malipo kwa ajili ya kukinunua akifika aendako akiangalia kitu alichokinunua na kukuta kipo tofauti na alivyokuwa akitarajia au kwa jinsi alivyovutiwa nacho kwa mara ya kwanza alipokiona anaweza kuvunjika moyo na hata kuthubutu kumrudishia aliyemuuzia.