Mtandao maarufu wa Twitter umetoa muonekano mpya wa picha kwa watumiaji wake wa kwenye kompyuta, muonekano huo utazifanya picha kuonekana katika saizi yake hata kabla hujazifungua.
Hapo mwanzoni Twitter walikua wanazipunguza ukubwa picha pindi zinapotokea katika ukurasa na ili uweze kuona picha vizuri basi ulihitaji kuifungua.
Pengine mabadiliko haya kwa Twitter sio kitu cha ajabu saana hasa ukizingatia kuwa toka mwanzo wa mwaka huu wamekuwa wakifanya mabadiliko katika mtandao wao, mabadiliko haya yote yanalenga kuifanya Twitter iweze kuhimili ushindani kutoka kwa mitandao kama Whatsapp Facebook Snapchat na Instagram.
Muonekano huu mpya wa Twitter utasaidia watumiaji kuweza kuona picha vizuri hata kabla ya kuzifungua kama ilivyokuwa huko mwanzo, pengine huu ni muendelezo tuu kufuatia mabadiliko ya huko nyuma ambayo yalifanya video kuweza kucheza bila ya kuwa naulazima wa mtumiaji kuicheza video hiyo maarufu kama autoplay.
Hii si habari nzuri kwa watumiaji wa Twitter ambao walikua wanaipenda Twitter ya zamani ile iliyokuwa ya maandishi matupu bila ya picha, hata hivyo kwa watu wa matangazo hizi ni habari njema maana hawatahitaji tena mtu kufungua tweet ili kusoma tangazo vizuri.
No Comment! Be the first one.