Samsung nii kampuni kubwa sana linalojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa simu, pia ina biashara zingine nyingi kama vile Tv n.k. Licha ya kuwa kampuni kubwa bado halijabeteka kwani kila siku linatafuta mbinu mpya ambazo zitalifanya kampuni hilo kubaki kuwa juu.
Hivi unakumbuka kuna kipindi simu za samsung ndio zilikua zinaongoza kwa mauzo duniani kote. Nazungumzia simu janja haswa zile za galaxy, Apple waliachwa na kampuni hii. Miaka ya 2011 mpaka 2013 kampuni la samsung lilitengeneza faida nyingi sana kupitia simu janja zake za samsung galaxy
Katika miaka hiyo samsung ilikuwa ni muuzaji bora wa simu janja kwa dunia na kuifanya Google (ALPHABET) kuwa ndio programu endeshaji bora kwa simu hizi (Android).
Samsung inaweza ikaja na mabadilko makubwa tuu kama ripoti zinazosikika sasa zitakuwa na ukweli ndami yale. Hivi sasa kuna fununu kuwa samsung gallaxy s7 kama ikija itakuja na punguzo la bei babkubwa, yaani itauzwa kwa bei ndogo kuliko samsung galaxy s6 inavyouzwa. Ndio! hili pekee linaweza badilisha mfumo mzima wa soko. Kumbuka bei ndogo sawasawa na wateja wengi kununua bidhaa,wateja wengi kununua bidhaa sawasawa na faida nyingi kwa haraka.
Pia kilichoishusha simu ya samsung kuwa kileleni ni ujio wa simu za Apple zile za iPhone 6 n 6+ (iPhone za kwanza zenye diplay kubwa).
Nchi kama china Samsung na iPhone hazina soko kubwa pengine labda watu wengi kule ni wa hali ya chini na simu hizi zina bei za juu (samsung na iPhone). China simu zinazoongoza kwa mauzo ni Xiomi na Huawei ambazo ni simu janja zenye bei ndogo.
Simu ya Samsung galaxy s7 inasemekana itatangazwa miezi ya karibuni, pengine mwezi wa kwanza. Najua wapenzi wengi wa samsung hawata ikosa hii. Lakini kumbuka ili samsung wawe juu inabidi walete kitu cha aina yake sokoni
One Comment