Katika nchi inayoongoza kwa uwepo wa teknolojia za ajabu ajabu katika maisha ya kila siku basi ni Japani. Utumiaji wa teknolojia za roboti katika vifaa mbalimbali umekuwa mkubwa sana. Leo vifahamu vyoo janja kutoka nchini humo.
Muonekano wa choo janja
Vyoo janja vya japani vitaongea na wewe, kukupa mziki, ‘massage’ na kisha kukusafisha baada ya haja kubwa na kwa wadada ata baada ya haja ndogo.
Kampuni kubwa ya nchini Japani, TOTO ndio kampuni mashuhuri zaidi inayotengeneza vyoo janja. Inasemekana katika vyoo vyote nchini Japani vyoo vinavyotumia teknolojia ya TOTO ni zaidi ya asimilia 65% ya vyoo vyote utakavyokutana navyo.
Kampuni ya TOTO inahistoria ya takribani miaka 33 katika utengenezaji wa vyoo na viti vya choo vinavyokuja na teknolojia ya WASHLET.
Viti vya kukaa vinakifaa cha kupachikwa kwa ajili ya kukalia na mfuniko wake wa kufunika na hapo ndipo TOTO wanakupa kifaa mbadala. Kufanya choo chako kiwe choo janja na teknolojia ya Washlet itakubidi ununue kifaa spesheli kutoka TOTO.
Kimombo sehemu ya kuweza kutoka na kubadilishwa kwenye vyoo vya kukalia inafahamika kama ‘Toilet seat’, yaani kiti cha choo. TOTO wametengeneza ‘toilet seat’ spesheli.
Kiti cha choo janja kinachotengenezwa na kampuni ya TOTO, kinaweza kutumika katika choo chochote cha kukaa
Kiti cha choo kutoka kwa TOTO kinakuja na eneo la upokeaji maji na pia waya unaotaji kuunganishwa na umeme. Kwa ufupi ni kwamba kutakuwa na laini mbili za maji, ya kwenda kwenye kuflashi choo na pia kwenda kwenye kiti cha choo chenye teknolojia ya WASHLET.
Umeme? Ndio, kifaa janja si kifaa janja bila uwepo wa umeme.
Kiti chako kinakuja na rimoti kwa ajili ya kukuwezesha kufanya mipangilio (settings) mbalimbali na kukusaidia kukiendesha choo hicho pale unapokitumia.
Mfanyakazi akionesha sehemu za bofya kwenye rimoti ya choo janja cha TOTO
Kiti cha choo kutoka kampuni ya TOTO kinachokuja na teknolojia ya Washlet kinasifa zifuatazo kwa ufupi kabisa;
Kutumia ‘sensor’ zake basi mfuniko wa choo utaweza kufunika na kujifunua kwa wewe kutumia rimoti au chenyewe chenyewe pale kikigundua mtu anakikaribia au anaondoka.
Kuna kibomba kidogo kinachochomoza na kuweza kukusafisha baada ya haja kubwa au/na ndogo (wadada) kwa kutumia maji ya vuguvugu kulingana na mapendeleo yako. Kibomba hicho kinakuwa kinajisafisha kwa maji moto kila baada na kabla ya kutumika. Kikishatumika kinavutwa na kufichwa eneo la ndani kidogo bila kuonekana.
Watu wengi hasa wa Marekani na kwingine waliozoea kutumia ‘TP’ – Toilet Paper zaidi suala hili la maji kuchomoza na kukusafisha haliwaingii akilini kabisa. Hasa wanaume!! 🙂
Mfumo wa kurusha maji ya vuguvugu kwa mtumiaji ili kumsafisha baada ya kujisaidia
Kifaa hicho kinachochomoza na kurusha maji kinaweza kuendeshwa kutumia rimoti kuweza kurusha maji katika eneo upendalo na kwa kasi gani na kwa joto gani.
Muonekano wa karibu wa kifaa kinachochomoza na kurusha maji ya kukusafisha. Kifaa hicho huwa kinaoshwa na maji ya moto sana kila baada na kabla ya kutumika
Kupitia rimoti yake utaweza pia kuweka kiasi cha joto ambacho ungependa kiti cha choo kiwe nacho. Hii ni muhimu kwa maeneo ya baridi kusaidia kuhakikisha ‘matako’ hayakutani na kiti chenye baridi sana pale unapokalia 🙂
Kiti cha choo kitaweza kupata joto kwa ajili ya maeneo yenye baridi zaidi
Sifa nyingine ni pia kila kabla ya kutumiwa na baada ya kutumiwa choo hicho hujimwagia maji yenye joto kali la kiwango cha kuua vijidudu vya aina yeyote kama sehemu ya kuhakikisha usafi upo sawa.
Kupitia rimoti unaweza bofya na kuleta sauti za milio mbalimbali kama vile miziki ili kusaidia kuficha sauti za zozote zinazoweza jitokeza ukiwa kwenye shughuli nzima ya kujisaidia haja kubwa.
Moja ya rimoti ikionesha sehemu mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na pa kuchezea mimbo, kuongeza na kupunguza sauti, kurusha maji ya kukusafisha n.k
Huduma ya ‘massage’ kwa matako yako… usicheke sana, ila ndio ukweli wenyewe. Kupitia rimoti yako utaweza kubofya na kupatiwa massage kutokana na mitikisiko (vibrations) taratiibu ya kiti cha choo.
Kiti hicho kina kina mfumo pia wa kuvuta hewa chafu wakati wote na kuichuja na kuisafisha kuhakikisha muda wote chooni panakuwa na hewa safi – kuondoa harufu kali
Mfumo wa kuvuta, kuchuja na kusafisha hewa ili kuondoa harufi kali kwenye choo
Pia baada ya kuoshwa choo janja hicho kitaelekeza hewa ya joto la kiasi flani ili kuweza kukukausha baada ya kusafishwa…kama utaona haitoshi basi unaruhusiwa kutumia TP kuweza kukausha unyevunyevu wowote uliobakia
Joto spesheli kwa ajili ya kukukausha baada ya kusafishwa
Je, una maoni gani juu ya teknolojia hii? Je, unaweza fikiria kununua na kutumia choo kama hichi? Ebu tuambie, pia unaweza angalia video fupi hapa chini inayoonesha utumiaji wa vyoo hivyo.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Mbunifu na mpenda teknolojia.
Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM
Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.
| mhariri(at)teknokona.co.tz |
No Comment! Be the first one.