Katika eneo la afya na mazoezi kuna App na mitandao mingi sana inategemea tuu na nini unataka kufanya kwa mwili wako kwa mfano kama vile kupungua, kukomaza misuli, kujikinga na maradhi, kujazia n.k. Kupata motisha (Kichocheo) kwa wanaotaka kufanya mazoezi peke yao nyumbani mara nyingine inakua ngumu ndio maana wengi hupendelea kufanya mazoezi kwa pamoja.
Mara nyingine ni vizuri kufanya vitu mwenyewe, Wewe ndio unaujua vizuri mwili wako na kama unajielewa vizuri hutahitaji hata mwalimu wa kukuambia nini ufanye. Unaweza tumia App mbalimbali au kuingia katika site zilizojikita katika mambo ya mazoezi
Kama hujui cha kufanya usijali kua App nyingi tuu zinaweza kukusaidia ili kujiweka fiti. Hapa kila kitu utafanya nyumbani hali hii pia haitakusaidia tuu kusevu hela zako bali pia itakuepusha na maisha ya Gym kama vile Kuchangia Bafu na Kuacha nyumba.
App Zipo Nyingi Lakini Hizi Ni Zile Za Umuhimu:
Fitnet:
Moja kati ya vile vitu vigumu ni kufanya mazoezi kwa kutumia video nyumani nani atagundua kama umeruka siku au hufanyi mazoezi hayo kama inavyotakiwa?. Fitnet ina shughulika na mambo yote hayo
Unaweza chagua mtu ambae atakua kama kocha wako katika mazoezi kutoka Fitnet. Kocha huyo atafuatilia maendeleo yako, atakupa kipeo na hata hamasa za kufanya mazoezi. Hii yote ni bure kwa wiki mbili za kwanza na baada ya hapo utalipia dola 19 za kimarekani kwa mwezi.
App ya Fitnet inatumia kamera ya simu, tabiti au laptop yako ili kupima kiasi gani unafanya mazoezi yako. App hii itaonyesha kakipande ka video pale juu kakikuonyesha ukiwa unafanya mazoezi yaaan app itakua inaku ‘sync’ wewe ukiwa unafanya mazoezi na kuonyesha kavideo kidogo kwa juu. Kama unafanya vizuri kutukua na vidoti vya rangi ya machungwa katika hiyo video. Video zote ni kuanzia dakika 3 mpaka 10.
Shusha Fitnet kwa Android au iOS
Sworkit:
Mara nyinigine njia bora ya kuanza kitu chochote ni kufanya. App ya Sworkit imejawa na mazoezi kibao na huhitaji hata vitendea kazi kutoka kwao. Cha kufanya ni kuseti mda ulikua nao na ni mazoezi gani ungependa fanya kwa mfanyo yale ya kujijaza mwili, yoga na kurefusha viungo.
Inaweza onekana ni kitu cha ajabu kufanya mazoezi ukielekezwa na simu yako na sio skrini kubwa, lakini Sworkit wanarahisha hilo. App inakuonyesha mazoezi gani ufanye na kwa mda gani utaweza kupanda daraja. Kwa uchaguzi wa mda unaoanzia dakika tano, hapa hakuna kisingizio cha kukufanya usitoke jasho kila siku
Shusha Sworkit kwa Android au iOS.
Change Collective:
Wakufunzi wa Change Collective hawakupi motisha wa kufanya mazoezi tuu bali lengo lao ni kukusaidia uishi maisha mazuri nje na ndani. Wanatoa kozi nyingi ambazo zinakua zikiendesha na video pamoja na ‘Podcast’ kutoka kwa wataalamu wa kila kitu kuanzia kwenye chakula mpaka kwenye kuamka asbuhi kufanya mazoezi. Kila siku itakubidi uingie katika App ili kupima maendeleo yako na kupata sapoti kutoka kwa wataalamu kwa kutumia sms au e-mail. System ya kozi hii itakupa motisha wa kutosha na kukufanya upende kuendelea na mazoezi.
FitStar:
Kama Sworkit vile, FitStar inatoa huduma ya mazozi mafupi mafupi ambayo unaweza fanya kwa muongozo kupitia simu yako. Katika App hii pia utaweza kufanyiwa mafunzo na mastaa wa NFL kama vile Tony Gonzalez katika video. kwa dola 40 za kimarekani utapata mafunzo marefu (mwaka mzima). Mafunzo ya mwaka (Fitstar Premium) yanakuja na machaguo mengi kama vile kuchagua jinsi unavyotaka mwili wako uwe. Unaweza fanya mazoezi haya bila vifaa na hata bila kutoa vitu vyote katika chumba ili upate nafasi.
Daily Burn:
Daily Burn ni App ambayo imeandaliwa na mkufunzi wa “Biggest Loser” Bw. Bob Harper, kwa hiyo unajua hii itakua ni siriazi. Hii inajumuisha siku 60 za kufanya mazoezi ya mwili. Mazoezi haya yapo kwa mfumo wa Harper anavyopendelea na anauita mfumo huo Black Fire (Moto Mweusi) lakini usiogope haitishi kama inavyosikika!
Harper alitengeneza App hiyo kwa mfumo wa aina yake kiasi kwamba hata kama ni mgeni katika mazoezi au umebobea katika mazoezi bado App hii itakufaa. Mda wako wa kufanya mazoezi itakua ni dakika 20 tuu na utahitaji baadhi ya vifaa lakini haimaanishi kuwa utahitaji chumba kikubwa ili kuweza fanya mazoezi haya. Huduma hii inapatikana katika Tv, Android na hata iOs au angalia kama kifaa chako kinaruhusu hapa
No Comment! Be the first one.