fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Intaneti Mtandao wa Kijamii simu Teknolojia

Majukwaa yanayotumika China

Majukwaa yanayotumika China
Spread the love

Unayafahamu majukwaa yanayotumika China? Kutokana na kuzuiwa kwa majukwaa mbalimbali pamoja na tovuti kutumika nchini China imepelekea makampuni ya teknolojia ya huko kutengeneza mbadala wa majukwa hayo ili wananchi wa huko waweze kutumia huduma zilizopo mtandaoni.

Kuna zaidi ya majukwaa 150 yaliyozuiliwa nchini china kwa sababu tofauti tofauti ikiwemo sababu za kiusalama na pia sababu za kimaadili. Baadhi ya majukwaa yaliyozuiliwa nchini China ni kama Google, Facebook, Youtube, Netflix, Wikipedia, Instagram na Whatsapp. Kuna baadhi ya majukwaa haya yamezuiliwa lakini yanaweza kutumiwa na watalii wakiwa katika maeneo mbalimbali ya kitalii nchini China.

SOMA PIA  Samsung watoa masasisho ya Android Pie kwenye Galaxy J7 Duo

Yafuatayo ni Majukwaa yanayotumika China 

Baidu: Ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa nchini China iliyobobea katika utoaji wa huduma na bidhaa zinazohusiana na mtandao pamoja na akili bandia (Artificial Intelligence). Kampuni hii inatoa huduma mbalimbali ikiwemo utafutaji wa huduma na taarifa mtandaoni kama ambavyo tunatafuta kupitia Google. Pia inatoa huduma ya ramani kupitia Baidu maps ambapo utaweza kuelekezwa kwenda sehemu mbalimbali kama kwenye Google maps.

Majukwaa yanayotumika China

Muonekano wa tovuti ya Baidu

WeChat: Ni mtandao wa kijamii wa kutuma na kupokea ujumbe papo hapo pamoja na kufanya malipo ya fedha kwa njia ya simu. Mtandao huu wa kijamii unamilikiwa na kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Tencent iliyopo nchini China. WeChat hutumika kama mbadala wa Whatsapp kwa wanachi wa China.

Majukwaa yanayotumika China

Muonekano wa WeChat

Youku: Hili ni jukwaa la kutuma na kuangalia video. Jukwaa hili linamilikiwa na kampuni kubwa ya kiteknolojia ya Alibaba Group nchini China. Unaweza kutuma na kuangalia video mbalimbali katika jukwaa hili na matumizi yake ni sawa na ya jukwaa la Youtube.

SOMA PIA  Njia Mbadala ya Kutumia WhatsApp kwenye Firefox kwa Kuona na Kujibu Ujumbe kwa Haraka

Weibo: Huu ni mtandao wa kijamii wa kusoma pamoja na kuandika makala fupi mtandaoni. Jukwaa hili linamilikiwa na kampuni ya Sina Corporation iliyopo nchini China. Matumizi ya jukwaa hili yanafanana na ya mtandao wa kijamii wa Twitter.

Zhihu: Hili ni jukwaa maalum kwaajili ya maswali na majibu linalotumiwa na wananchi wa China. Jukwaa hili linamilikiwa na kampuni ya kiteknolojia ya Zhihu Inc iliyopo nchini China. Matumizi ya jukwaa hili yanafanan na ya jukwaa la Quora.

SOMA PIA  JIEPUSHE Na Ku'click 'Link' Zisizo Na Maana Kwenye Mitandao Ya Kijamii!!

Kama umefurahishwa na makala hii usiache kutoa maoni yako kwa ku comment hapo chini. Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kufahamu zaidi mambo mbalimbali kuhusu teknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania