fbpx

Uwezo wa kuomba kujiunga kwenye video mubashara kwenye Instagram

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kipengele cha video za papo kwa papo kwenye mitandao ya kijamii ni moja kati ya vitu ambavyo vimefanya mitandao ya kijamii izidi kuvutia kutokana na uwezo wa kuonyesha kile kinachoendelea eneo fulani aidha kwa mfumo wa sauti/picha za mnato na kuonekana kuwa na umuhimu wake.

Instagram, moja ya mtandao wa kijamii wenye watumiaji wengi zaidi duniani na sasa imeongeza kitu kipya kwenye app yake pale mtu anapochapisha video mubashara kwenye akaunti yake ya Instagram. Hapa namaanisha rafiki wa aliyechapisha video mubashara anaweza kuomba kujiunga kwenye hiyo picha jongefu ambayo ni mubashara uliyochapisha kwenye akaunti ya Instagram au kwa lugha rahisi ni kujiunga kwenye live chat. Unaweza KUBOFYA HAPA! kujua zaidi kuhusu live chat.

Kipengele cha kuweza kuomba (request) kujiunga kwenye video ya papo kwa papo kutoka kwa rafiki kwenye Instagram.

Katika sasisho hilo kwenye programu tumishi ya Instagram inamuwezesha rafiki kuomba kujiunga kwenye video ya papo kwa papo (mubashara) kwa kutuma maombi kupitia kwenye sehemu ya kuandika maoni.

Instagram imeongeza kipengele cha rafiki kujiunga kwenye video ya papo kwa papo kutoka kwa rafiki yake.

Kama aliyechapisha video hiyo mubashara akikubali ombi lililotumwa na muombaji muonekano wa video hiyo unagwanyika kulingana na idadi ya watu waliokubaliwa kujiunga kwenye video hiyo ya papo kwa papo.

Masasisho hayo ni kote (kwenye Android pamoja na iOS) na si lazima umkubali aliyeomba kujiunga kwenye video yako ya papo kwa papo. Pia, ni lazima muombaje awe amemfuata kuweza kutuma ombi la kujiunga kwenye video mubashara. Tuambie, unalionaje sasisho hilo jipya kwenye Instagram?

Vyanzo: The Verge, AD Week

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Waanzilishi Wa Mtandao Wa Vine Waja Na Mtandao Mwingine, Hype!
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|