fbpx

Motorola One na One Power ndio hizo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Wiki hii imekuwa ni simu baada ya simu kwenye maonyesho ya IFA 2018 huko Berlin-Ujerumani na moja ya rununu iliyoletwa machoni pa watu ni Motorola One na One Power.

Makampuni mbalimbali yamekuwa yakitumia mkutano huo kutoa simu janja ambazo safari hii angalau kwa simu ambazo tumeshazizungumzia bei zake ni stahimilivu (sio ghali) zikiwemo Motorola One/One Power ambazo zimetoka kwa pamoja.

Motorola One na One Power

Jicho la karibu kwa Motorola One ambayo ina umbo la “V” kama ilivyo kwenye iPhone X.

Katika mchanua wa leo nimeamua nichambue simu hizi katika namna rahisi na nyepsi ambayo itakuwa ni rahisi kueleweka:

Kipengele

Motorola One

Motorola One Power

RAM GB 4 GB 4
Mega Pixels (MP) Kamera ya Mbele: 8MP na Kamera za Nyuma: Zipo 2; MP 13+2MP Kamera ya Mbele: 12MP+LED flash na Kamera za Nyuma: Zipo 2; MP 16+5MP pamoja na LED flash 2
Picha jongefu Ina uwezo wa kurekodi picha mnato zenye ubora wa 4K. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato zenye ubora wa 4K.
Uwezo wa Betri 3000mAh, halitoki pia linakaa na chaji kwa siku nzima pia ina teknolojia ya kuchaji haraka; inachukua dakika 20 tu kujaa chaji. 5000mAh, halitoki pia linadumu na chaji kwa muda wa siku mbili (kwa matumizi yoyote). Vilevile, ile teknolojia ya kuchaji simu haraka inachukua robo saa kulifanya betri liwe limejaa.
Kipuri mama Qualcomm Snapdrago 625, kasi yake ni 2 GHz Qualcomm Snapdrago 636, kasi yake ni 1.8 GHz
Mawasiliano GSM / HSPA / LTE GSM / HSPA / LTE
Memori ya Ndani GB 64 GB 64
Memori Kadi? Inaruhusu kuongeza mpaka GB 256 Inaruhusu kuongeza mpaka GB 256
Uwiano wa kioo 19:9 19:9
Aina Ya Kioo IPS (LCD) IPS (LCD)
Ukubwa Wa Kioo Inchi 5.9 Inchi 6.2
Utambuzi Wa Alama Za Vidole? Ndio – Upo Kwa Nyuma Ndio – Upo Kwa Nyuma
Rangi Nyeusi
Nyeusi
Ukubwa (Wembamba) 150 x 72.2 x 8.0mm Sm 17.5
Muonekano  Umbo lake linatengenezwa na kioo (Gorilla 2.5 pande wa nyuma na mbele) pamoja na chuma. Kuna sehemu ya kuchomekaspika za masikioni. Umbo lake linatengenezwa na kioo (Gorilla 2.5 pande wa nyuma na mbele) pamoja na chuma. Kuna sehemu ya kuchomekaspika za masikioni.
INAYOHUSIANA  Ubora wa picha kwenye Nokia 9 PureView

Simu zote mbili zinatumia Android 8.1 Oreo (Android One), simu zote zitapokea masasisho ya kuhamia kwenye Android 9 Pie katika siku za usoni na Google wameahidi kutoa masasisho ya kuzilinda simu hizo katika kupindi cha miaka mitatu.

Motorola One na One Power

Motorola One Power.

Motorola One inauzwa kwa karibu $347|Tsh. 798,100 na Motorola One Power bei yake bado haijatangazwa ikitazamiwa kuanza kupatikana duniani kote kuanzia mwezi Oktoba.

Vyanzo: CNET, The Verge, Engadget, XDA

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.