fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android Android Pie simu Teknolojia

Undani wa toleo jipya la Android 9 Pie

Undani wa toleo jipya la Android 9 Pie

Spread the love

Google imetangaza rasmi toleo lake kubwa lijalo la Android juma lililopita likiitwa Android 9 Pie.

Toleo hili lipo tayari kwa mageuzi mapya likiwa katika muundo imara na limeanza kupatikana kirahisi kwa watumiaji kwa kupakua kupitia baadhi ya simu za Google Pixel.

Android Pie ni toleo kubwa la tisa la Android na sasa linachukua nafasi ya toleo la mwaka 2017, Android 8 (Oreo).

toleo jipya la Android

Nembo inayoitambulisha Android Pie.

Toleo hili lina vitu kadhaa vipya, huku msingi wake ukijikita katika kuwezesha na kutambua haraka namna ya kuifanya simu yako ifanye kazi kwa ufanisi zaidi. Undani wa vipengele vilivyopo kwenye Android Pie ni kama ifuatavyo:-

Adaptive Battery

Miongoni mwa sifa mpya ni kishabihishi cha betri (Adaptive Battery) ambacho hung’amua kwa ufanisi, ni programu tumishi zipi unazitumia kwa uchache na hivyo kuzikatia umeme ili kuliwezesha betri kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi.

SOMA PIA  Fahamu: Korea Ya Kaskazini wana Mfumo-Endeshaji Wa Kipekee

Adaptive Brightness

Vivyo hivyo, kishabihishi cha mwanga (Adaptive Brightness) kitarekebisha chenyewe mwangaza sahihi kwenye kioo cha simu kulingana na mahali ulipo kwa wakati husika  pia kitu gani unachofanya kwenye simu yako.

toleo jipya la Android

Teknolojia ya kupunguza/kuongeza mwanga iliyoboreshwa kwenye Android Pie.

Slices

Sifa nyingine mpya kabisa katika toleo hili ni kuwapo kwa ‘Slices’, ambapo  programu mbalimbali kujisogeza karibu hivyo kuweza kupata kitu unachotafuta kwa haraka.

Kwa mfano, ikiwa unatafuta “Lyft” kwenye Playstore, programu husika itaonyesha pia ‘Slice’ pamoja na programu nyingine maarufu.

toleo jipya la Android

Kipengele cha “Slices” kinavyosaidia kuweza kutafuta kitu kwa haraka zaidi kwenye Android 9.

Uwezo wa kutafuta kitu

Android Pie pia inaingiza rasmi mfumo mpya wa ‘navigation’. Kazi za vitufe vitatu vya chini havipo tena na badala yake kipo kitufe kimoja tuu ambacho kinaweza kusogea huku na kule.

SOMA PIA  Apple Yazidiwa Na Android Huko Nchini India!

Mathalani ukipangusa kwa haraka kutokea kitufe cha nyumbani kwa kwenda juu itakupeleka kwenye programu tumishi ambazo umezifungua, ukishikilia kwa sekunde kadhaa kwa kwenda chini utakuwa umewasha kipengele cha Google Assistant.

Pia miito ya ujio wa taarifa fupi imeboreshwa huku mfumo wa sasa ukipanuliwa kwa kuwa na chaguo thabiti za kujibu ujumbe papo kwa papo (smart reply options).

Kwenye toleo hili la sasa vifupisho hivyo vinatakakiwa viwekwe kupitia mpangilio; Settings > System > Gestures and toggle.

Digital Wellbeing

Simu zitakazohamia toleo la Android Pie pia zitakuwa na kipengelekiitwacho ‘Digital Wellbeing’ ambacho kinahusisha ukurasa wa mwanzo wa kipengele hicho (Dashboard) ukaoonyesha mwenendo wa simu yako:

SOMA PIA  Western Digital Mbioni Kuinunua SanDisk Kwa Dola Bilioni 19!

katika matumizi ya programu tumishi, kuweka muda maalum (App Timer) kuzuia matumizi kupita kiasi (kuzuia uraibu), ‘Wind Down’ ambacho kitawasha taa usiku na kutokusumbua kwa kioo kubadilika rangi na kuwa kama ya kijivu ili kutoendelea kutumika kupita kiasi kwa simu wakati wa kulala.

toleo jipya la Android

Kwenye Android 9 inakupa uwanja mpana wa mtu kuweza kujipangia muda ambao atataka kutumia programu tumishi na saa ikitimia tu basi programu husika inaondoka hewani.

Volume Slider

Pia kuna mabadiliko ya ishara ya kupunguza/kuongeza sauti ambapo sasa itapatikana upande wa kulia wa simu yako badala ya juu pale unabobonyeza Batani ya sauti kwa ajili ya kupunguza au kuongeza sauti.

toleo jipya la Android

Ukiwa unaongeza/kupunguza sauti kwenye Android 9 sasa utaona kinachofanyika kutoka upande wa kushoto wa kioo cha simu.

Muonekano wa simu kuzungukazunguka

Kwenye Android 9 sasa utaweza kuona alama ya kuonyesha kuwa umefunga ili isizungukezunguke utakiona upande wa juu kabsa kama kielelezo kuwa kipengele hicho kinafanya kazi yake.

toleo jipya la Android

Pia hata sehemu ambapo saa ilikuwa imewekwa kwa toleo lililopita (upande wa kulia) mambo yamebadilika kidogo na hivi sasa ukitaka kutazama muda itabidi upeleke macho yako upande wa kushoto juu.

Kwa sasa toleo la Anroid Pie linapatikana kwa simu za Pixel kwa toleo la majaribio na kwa simu zingine litapatikana kwa ukamilifu hapo baadae.

Pia zipo sifa nyinginezo kuhusiana toleo hili jipya ikiwamo mifumo iliyoboreshwa ya usalama wa simu, lakini yote hayo tutayaangazia kiundani siku nyingine hapa hapa TeknoKona.

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania