Huawei AppGallery duka la tatu kwa ukubwa baada ya Play Store na App store

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Hivi karibuni Huawei ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Duka lake la programu la AppGallery litakalokuwa kwenye simu zake za Huawei. Taarifa kutoka Huawei zinasema AppGallery ya sasa limekuwa duka kubwa la tatu duniani baada ya Android(Play store) na Apple (App store).

AppGallery imekuja baada ya zuio la Marekani kwa Huawei kutotumia App za nchi hiyo ikiwemo Play Store inayobeba programu nyingi maarufu.

INAYOHUSIANA  Utafiti: Snapchat ndio mtandao unaoongoza kutumiwa na vijana Marekani

huawei appgallery

Tangu uzinduzi wa AppGallery Huawei imekuwa ikiwavutia watengenezaji wa program mbalimbali duniani kuweza kuweka programu zao kwenye Duka hilo. Aidha watumiaji wa AppGallery wamekuwa wakiongezeka kufikia milioni 400 kwa mwezi na kukiwa na zaidi programu 55,000 ndani ya AppGallery.

Huduma ya AppGallery inapatikana katika nchi 170 na ikishirikiana na watengenezaji wa App kutoka  Asia, Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, na Amerika ya Kusini.

huawei appgallery

Watengenezaji apps wananufaika zaidi katika app ya App Gallery kwa kupata asilimia 90 ya mauzo. Kumbuka kwenye app ya Google PlayStore mtengeneza app inayouzwa anapata asilimia 70 tuu ya mauzo nyingine zikienda kwa Google

Kampuni hiyo pia ilitangaza kuwa itakuwa na uzinduzi wa “Quick App”, huduma ambayo itawawezesha watumiaji kujaribu/kutumia programu bila ya kuwa na haja ya kudownload na kuinstall. Hii itasaidia kwa simu zenye uhifadhi mdogo.

INAYOHUSIANA  SAMSUNG GALAXY S3: Simu ya Android Iliyosubiliwa Kwa Hamu

Taratibu Huawei wanaanza kujijenga kuepukana na ukiritimba wa utawala wa Marekani katika Teknolojia.

Unaweza kupakuwa na kuweka AppGallery katika simu yako yoyote ya mfumo wa android kwenye Link hapo chini.

AppGallery

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.