fbpx
Afya, ALPHABET, Google

Wafanyakazi Google kufanya kazi wakiwa nyumbani. #Coronavirus

wafanyakazi-google-kufanya-kazi-wakiwa-nyumbani-coronavirus
Sambaza

Wafanyakazi wa Google wanaungana na wafanyakazi wa makampuni mengine makubwa ya teknolojia nchini Marekani katika kufanya kazi za kiofisi wakiwa nyumbani. Kutokana na kuendelea kwa kusambaa kwa ugonjwa wa kirusi cha Corona uamuzi huu unaonekana ni muhimu kwa kampuni hiyo.

Agizo hilo limetolewa kwa takribani wafanyakazi 100,000 wa kampuni hiyo nchini Marekani na Kanada, na linawahusu wafanyakazi wa makampuni yote yaliyo chini ya kampuni mama ya ALPHABET inayomiliki Google. Makampuni mengine ambayo yameshachukua uamuzi huo, wengine kwenye baadhi miji na wengine nchi nzima ni pamoja na Apple, Amazon, Microsoft na Facebook.

INAYOHUSIANA  Simu ya Pixel 3A na 3A XL - Google waja na Simu ya Pixels kwa bei 'rafiki'
google coronavirus  kufanya kazi wakiwa nyumbani
Google: Wafanyakazi kufanya kazi wakiwa nyumbani

Amazon na Facebook tayari ina wafanyakazi waliokutwa na maambukizi hayo.

Mlipuko wa ugonjwa huu umeleta hasara kubwa katika masoko ya hisa la Marekani na ya mataifa mengine. Makampuni hasa ya teknolojia yanayotegemea malighafi na vipuri kutoka mataifa mengine, na yanayotegemea biashara zinazohusisha mahitaji ya kusafiri yote yameathirika sana kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa huu.

Tayari mikutano na maonesho mbalimbali ya kiteknolojia yaliyokuwa yamepangwa kufanyika katika maeneo mbalimbali Marekani na katika mengine ya Ulaya yameshaairishwa na mengine kusogezwa mbele.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |