fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Microsoft Teknolojia Windows 11 Pro

Kutumia Windows 11 Pro kuhitaji akaunti ya Microsoft

Kutumia Windows 11 Pro kuhitaji akaunti ya Microsoft

Spread the love

Toleo jipya la programu endeshi kutoka kwenye familia ya Windows inapata wateja kwani kompyuta nyingi sasa watu wanaamua kubadilisha na kuweka kitu kipya. Windows 11 Pro ni toleo mojawapo la programu endeshi ambazo zipo chini ya Windows na zinafanya kazi bega kwa bega na Microsoft.

Watu wengi ambao wanatumia kompyuta hivi sasa wengi wao utakuta wameweka Windows 11 bila kujali kama kifaa hicho kimekidhi vigezo vya kuweza kutumia toleo hilo la programu endeshi. Ukweli ni kwamba wengi hawajali na wanasonga tuu na ingawa kompyuta inatumika lakini kuna masasisho ambayo kompyuta haiweza kuyapokea kutoka Microsoft kutokana na kutokuwa na zile sifa walizoziweka wnyewe.

SOMA PIA  Youtube yazidi kuwawekea ngumu wenye msimamo mkali

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba kuweka Windows 11 Pro kwenye komputa basi itamlazimu mtu kuingiza akaunti ya Microsoft (Hotmail/Live) ili kuweza kuendelea na mchakato wa kuifanya progrramu endeshi ianze kutumiaka na hapa maana yake pia itahitajika intaneti ili kuwezakufanikisha kuingiza/kutengenza akauntiya Microsoft iwapo mhusika hana.

Windows 11 Pro

Ulazima wa kuwa na akaunti ya Microsoft ili kuweza kutumia Windows 11.

Ulazima wa kuwa na akaunti ya Microsoft umeonekana pia kwenye Windows 11 Home Edition ambayo inahitaji mtu kuweka akaunti ya Hotmail au Live ili aweze kumaliza mchakato wa kuifanya programu tumishi ianze kutumika.

SOMA PIA  Microsoft Azure ni nini hasa? #Teknolojia #DoMore

Miezi ya nyuma huko wajanja walikuwa wanatumia mbinu ya kuondoa intaneti halafu wanatengeneza akaunti ya kawaida tuu (ya humohumo ndani kwa ndani) lakini hilo sasa linakwenda kufikia ukomo hivyo kufanya kuwa na ulazima wa kuwa na/kutengeneza akaunti ya Microsoft ili kufanya programu endeshi itumike.

Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] Windows 11 ni programu endeshi ambayo inawika sehemu nyingi duniani na inachagizwa na upya wake kitu ambacho watu wengi ulimwenguni wanaweka toleo hilo kwenye kompyuta zao bila kujali kifaa husika kimekidhi vigezo vya kuwa na sifa zinazohitajika kuwa katika sehemu salama ya kupakua masasisho yanapotoka. […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania