TeknoKona tumeshaandika makala kuhususiana na sifa gani kompyuta inatakiwa kuwa nazo ili kuwa na uwezo wa kukubali Windows 11 hata hivyo wapo wale ambao wataishusha na kuiweka kwenye vifaa vyao tuu.
Microsoft wameshaweka wazi kuwa kompyuta mbalimbali (hata zile za zamani) zitaruhusiwa kuweza kuiweka programu hiyo endeshi ambayo bado haijatoka rasmi ingawa kuna baadhi ya watu maeneo mbalimbali duniani wameshajaribu kutumia Windows 11 kwenye kompyuta zao.
Katika kutambua kuna wale wenzangu na mimi ambao wataishusha tuu na kuweka Windows 11 kwenye kompyuta basi nikaona nitoe elimu hii. Swali la kwanza kabla ya kutaka kushusha Windows 11 unapaswa kujiuliza kompyuta yangu inakidhi vigezo vilivyowekwa na Microsoft? Kama huna uhakika ama unataka kujiridhisha zaidi basi ni vyema ukapakua programu wezeshi iitwayo PC Health Check ambayo itakupa majibu unayotafuta.
Shauku ya kutaka kujua iwapo kompyuta yangu imefikia kiwango
Mara baada ya kupakua pprogramu wezeshi-PC Health Check nikata kufahamu iwapo kompyuta ninayotumia itaweza kufanya kazi vizuri ikiwa na Windows 11. Kiukweli nilipata majibu chini ya sekunde 3 mara baada ya kubonyeza kitufe kilichoandikwa “Check now” na kuelezwa kinagaubaga.
Kompyuta ambayo nimetumia kujua iwapo itafaa kuwekwa Windows 11 haijakidhi vigezo jambo ambalo inanibidi kufikiria kubadilisha na kununua iliyo bora zaidi kwani maisha ya Windows 10 huenda yakawa yanafikia ukingoni hadi kufikia mwaka 2025 huenda tusipokee masasisho muhimu kutoka Microsoft. Kwa maana hiyo nguvu kubwa itakuwa kwa wale ambao kompyuta zao zinatumia Windows 11.
Je, kompyuta uliyonayo/unayotumia ina uwezo wa kufanya kazi vyema kwenye Windows 11? Pakua programu wezeshi kwa KUBOFYA HAPA kuweza kujua.
TeknoKona kama kawaida yetu tumeendelea kukuhabarisha lakini pia kukuelimisha hivyo basi tukusihi usiache kutufuatilia kila siku tunapojaliwa pumzi ya uhai.
Vyanzo: Engadget, Windows central, mitandao mbalimbali
3 Comments