fbpx
Android, apps, Facebook, iOS, Mtandao wa Kijamii, Teknolojia, whatsapp

Kutoka WhatsApp Status mpaka kwenye Facebook Stories

kutoka-whatsapp-status-mpaka-kwenye-facebook-stories
Sambaza

Katika ulimwengu wa teknolojia na hasa mitandao ya kijamii kwa miaka ya karibuni ukizungumzia WhatsApp status au Facebook stories sio vitu vigeni machoni pa watu. Facebook ambao ndio wanamiliki WhatsApp wanataka kuongeza ushirikiano kwenye programu tumishi husika.

Katika matumizi yako ya kila siku kwenye WhatsApp/Facebook ninaamini kuwa huwa unapitiapitia yale ambayo marafiki, ndugu, n.k hapa nikimaanisha machapisho ya watu kwenye WhatsApp status/Facebook stories au vyote viwili. Basi fahamu ya kuwa Facecbook wapo kwenye mjaribio ya kuwezesha kile ambacho utakiweka kama WhatsApp status ukipenda utaweza kuchapisha kitu hicho hicho kwenye Facebook stories, Instagram, Gmail, Google Photo.

INAYOHUSIANA  Meizu Zero: Simu isiyokuwa na mengi tuliyoyazoea
Facebook Stories
Uwezo wa kuchapisha kitu kilekile kutoka kwenye WhatsApp status kwenda Facebook stories.

Kitu hicho kipya kimeonekana kwenye WhatsApp Beta kwa maana ya kwamba bado katika hatua za majaribio na pengine ikipata mrejesho mzuri huenda ikaruhusiwa kuja kwa watumiaji wengine wote wa Android/iOS.

Facebook stories/WhatsApp status ni vitu viwili vinavyofanana lakini sehemu mbili tofauti; zote zinafanya kazi ya kuchapisha vitu ambavyo vinadumu kwa saa 24 tu! na baada ya hapo vinatoweka mara moja tayari kwa chapisho jingine.

Facebook Stories
Facebook wanataka kurahisisha mambo kuwezesha watumiaji wake kuchapisha kitu kimoja sehemu mbili tofauti.

Watu ambao mnatumia toleo la majaribio-WhatsApp Beta sina shaka mtakuwa mmeshayaona mabadiliko hayo kama bado basi unatakiwa kupakua toleo la karibuni kabisa ili kuwa miongoni mwa wale wanaopata masasisho kabla ya watumiaji wengine wote wa WhatsApp.

Vyanzo: GSMArena, The Verge, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|