fbpx
Android, apps, iOS, whatsapp

Amua nani akuweke kwenye kundi #WhatsApp

amua-nani-akuweke-kwenye-kundi
Sambaza

Mawasiliano kwenye kikundi ndani ya WhatsApp sio kitu cha ajabu kabisa na kila mara makundi mbalimbali yanaundwa na watu wanaongezwa huko. Swali ni je, ungependa uweze kuamua nani akuweke kwenye kundi?

Tukianza kutafuta idadi kamili ya makundi yaliyopo kwenye WhatsApp kwa kila mtumiaji wa programu tumishi inayotumiwa na watu wengi zaidi duniani itakuwa ni jambo ambalo halitawezekana kiurahisi na pengine lisiwezekane kabisa. Kwa muktadha huo watu wengi hawapendezwi na suala la kuunganishwa kwenye kundi fulani bila kujua/kupewa taarifa kabla jambo hilo kufanyika.

INAYOHUSIANA  Mambo 11 Yakushangaza Kuhusu Virusi vya Kompyuta

Ukiwa mpekuzi mzuri WhatsApp utaweza kuwa umegundua kuwa unaweza ukaamua ni akuweke kwenye kundi ndani ya programu tumishi husika au usiruhusu mtu yeyote kuweza kukuweka kwendi kundi, kama ulikuwa hufahamu basi fahamu leo!. Swali la pili ambalo pengine utajiuliza ni nini ufanye ili kufanikisha?. Fanya vitu vitu vifuatavyo:-

ingia Settings > Account > Privacy > Groups kisha chagua “Everyone” iwapo utapenda yeyote yule awe anaweza kukuunga kwenye kundi au “My contacts” (namba za simu ulizozihifadhi kwenye simu janja yako) kwa maana ya kwamba wao tu ndio watakuwa na uwezo wa kukufanya kuwa mwana jumuiya ndani ya kikundi fulani na kama hutapenda kuunganishwa kwenye kundi lolote lile ndani ya WhatsApp utachagua “Nobody“.

akuweke kwenye kundi
Kuwa mwamuzi nani awe anaweza kukuunga kwenye kikundani ndani ya WhatsApp. Vilevile, kwa yule ambae itashindikana kuongeza utaweza kumtumia ombi la kujiunga ambalo litadumu kwa saa 72 pekee.

Haya sasa kwa uwamuzi wa kuwekwa au kutowekwa kwenye kikundi WhatsApp upo ndani ya uwezo wako kabisa kwa kufuata hatua ambazo zimeelezwa hapo juu. Vipi unafurahishwa na kipengele hicho ndani ya programu tumishi hiyo?

Vyanzo: Life Hacker, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|