Kwa miezi kadhaa watumiaji wa WhatsApp wamekuwa kwenye wakati mgumu mara baada ya kutoka taarifa ambayo itawataka kukubaliana na masharti ya WhatsApp ndio waweze kuendelea kutumia akaunti zao.
Kama utakuwa ni mtu ambae unafuatilia masharti ya matumizi ya WhatsApp ama “Terms of Service” walisema kuwa wasingefuta akaunti ya WhatsApp iwapo mtu asigekubaliana na masharti mapya ila mtu huyo atakuwa anapata baadhi ya huduma katika hali isiyo ya ukamilifu. Lakini wiki chache baadae WhatsApp wakaamua kutowabana mambo na waweze kutumia programu tumishi hiyo kikamilifu.
Kwa mujibu wa WaBetaInfo WhatsApp wanasema si lazima kwa mtu kukubaliana na masharti yao mapya ili kuweza kuendelea kutumia WhatsApp lakini iwapo utawasiliana na mtu anyetumia akaunti ya biashara inayotumia huduma za utunzaji wa vitu “Kusikojulikana” (cloud services) itamlazimu mhusika kuweza kukubaliana na maelezo kuhusu matumizi ya WhatsApp ili ujumbe wake uweze kumfikia aliyekusudia kumtumia.

Taarifa kuhusu hakuna ullazima wa kukubali masharti itarajiwa kuja rasmi kwa watumiaji wote wa WhatsApp katika maboresho yatakayotoka katika siku za usoni. Ni wakati wako sasa kutumbia ewe msomaji wetu iwaapo umependezwa na habari hii au la!
Leo ni siku nyingine na daima tunakusihi kuendelea kutufuatilia kwani tupo hapa machweo na mawio kukuhabarisha masuala mablimbali ya teknolojia.
Chanzo: WaBetaInfo
No Comment! Be the first one.