Swiftkey ni huduma ya keyboard katika vifaa mbalimbali ikiwemo simu na vifaa vingine kadha wa kadha, kwa sasa huduma hii katika vifaa vya iOS iko tamati.
Ifahamike kuwa huduma hii inamilikiwa na kampuni ya Microsoft ambayo ndio ina mamlaka juu ya maamuzi yote kuhusiana na Swiftkey.

Kinachofanyika ni kwamba kampuni ya Microsoft inaiondoa kabisa Swiftkey katika soko la App la App Store na vile vile inaacha kutoa huduma za kimsaada (Support) katika toleo la iOS la App ya keyboard hiyo.
Hili litafanyika kuanzia oktoba tarehe 5, lakini kingine ni kwamba kama utakua nayo katika simu bado utaendelea kuitumia kama kawaida tuu mpaka utakapoifuta mwenyewe.

Kwa watumiaji wa Android wao wataendelea kutumia App hiyo kama kawaida tuu na wao hawataguswa kabisa na jambo hili ambalo linaenda kutokea tarehe 5.
Zoezi hili zima limekuja baada ya kampuni kupata malalamiko fulani kwa watumiaji wa iOS, malalamiko ambayo hawakuyapatia majibu, kingine ni kwamba hata sasisho la kawaida tuu halijawahi kutokea kwa watumiaji wa iOS zaidi ya mwaka.
Swiftkey imekua ikipatikana katika App Store tangia mwaka 2014 (2016 Microsoft ikainunua), japokuwa kulikua na ishara nyingi kwamba kampuni imeachana na Swiftkey katika iOS kimya kimya.

Ukiachana na yote haya ni kwamba bado kuna swali ambalo Microsoft wenyewe hawajaweka wazi juu ya kwanini wanaachana na App hiyo katika upande wa iOS.
Naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unaona ni sawa kwa Microsoft kufanya jambo hili tena bila ya kutoa maelezo ya kutosha kwa watumaiji wa iOS na wengine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.