Kama unahisi teknolojia ya vioo vya kujikunja haijakuacha mdomo wazi pengine hii inaweza ikakufanya hivyo, kwa sasa Samsung na kampuni ya Intel inaangia jikoni katika kuhakikisha inazalisha kompyuta…
…Pengine ikawa kompyuta ya kwanza ambazo inaongezeka ukubwa kwa kuongezwa hapo hapo, yaaani kwa mfano kioo hichi cha Samsung na Intel kinaweza kuwa nchi 7 na kikaongezwa hapo hapo mpaka kufikia nchi 10.
Ngoja kwanza usichanganyikiwe yaani ni hivi kompyuta hiyo itakua na uwezo wa kujiuongeza upana na kuwa na umbo kubwa, umbo hilo litahusisha mpaka kioo.
Mkuu wa kitengo cha vioo katika kampuni ya Samsung, bwana JS Choi alionekana katika jukwaa akiwa anatambulisha kifaa hiki kwa kutumia kompyuta ambacho sio rasmi (mfano).

Tabati hiyo ilitoka kuwa na ukubwa wa Inchi 13 na kuongezeka/kuongezwa mpaka kufikia kioo cha Inchi 17, jambo ambalo linaliwavutia wengi sana.
Kwa haraka haraka ni kwamba teknolojia hii iko mahususi zaidi kwa kompyuta mpakato au hata katika tabiti na sio mahususi sana kwa vifaa vingine.

Pata picha uwezo wa kuweza kuongeza ukubwa wa kioo cha kifaa kwa kusukuma pembeni tuu, hii itakusaidia na kukupa picha nzuri kama utakua unaagalia video au unafanya vitu vingine ambavyo vinahitaji uso mkubwa wa kioo.
Wakati makampuni mengine makubwa tuu hajaingia hata katika teknolojia ya vioo vya simu vya kujikunja kama Samsung, tayari kampuni limeshahamia katika teknolojia nyingine ambayo vilevile itakua ya mapinduzi makubwa sana.
Intel katika teknolojia ya kompyuta ni bingwa kabisa na ukizingatia kwa ushirika huu wa Samsung ni wazi kabisa kwamba watakuja na kitu kizuri kabisa.
Mpaka kufkia sasa jambo hili lipo katika wazo picha kabisa na kwa kulingana na utendaji kazi wa kampuni zote hizi mbili inawekana bidhaa hii ikawahi kuingia sokoni.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje na je uko tayari kuanza kutumia kifaa chenye teknolojia hii?`
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.