Mouse ni kitu muhimu sana katika kompyuta zetu, hata laptop. Saa nyingine kutumia mouse ya kwenye laptop inaleta shida kidogo na haswa pale ukiwa unatumia programu inayohitaji kutumia mouse na keyboard kwa sana kama vile Adobe Photoshop.
Kompyuta imeboresha maisha yetu kwa kiasi kikubwa sana kulinganisha na nyakati za zamani. Siku hizi mtu unaweza andika vitu mbalimbali ikiwemo E-mail, memo na avitu vingine mbalimbali jwa kutumia komoyuta yako, sasa hebu fikiria kuyafanya hayo yote kwa kutumia peni (ushachoka tayari sio?)
Licha ya kuwa zimetuboresha ki ujumla lakini bado kompyuta ina vitu fulani fulani ambavyo vinaweza vikapunguza kasi yetu wakati tunaitumia. Kitu kimoja wapo ni Mouse ya kompyuta yako.
Kama unatumia Desktop sawa Mouse yenye kitairi inaweza ikawa ndio chaguo zuri maana unaweza pandisha na kushusha kurasa kama Facebook, Twitter na nyingine nyingi bila shida yeyote, na unaweza fanya sawa sawa na software zingine kama zile za Microsoft office
Sema matumizi ya Mouse hizi yanaishia pale pale (tulipo pazoea) vipi kama unaweza fanya mouse hizi kuwa na matumizi mengi kuliko tuliyo yazoea?
Kwa mfano kama umefungua windows mpya juu ya nyingine kurudi kwa ile ya mwanzo itakubidi ufunge hii mpya, uifiche kwa chini au uipunguze ukubwa — sasa hayo yote ya nini — hapo unaweza ukapoteza muda
Kwa kutumia WizMouse unaweza ukafanya mambo mbali mbali kipekee kabisa kwani ni ya aina yake
Ukishafanikiwa kuweka WizMouse katika kompyuta yako haitakuhitaji kuanza kufungu au kufunga window nyingine, itakubidi kutumia kitairi cha mouse yako tuu. WizMouse ni kwa ajili ya kuongeza urahisi wa maisha yako katika kompyuta
Click Hapa ili kupelekwa katika tovuti ya antibody-software ambapo utakutana na faili la WizMouse. Fuata maelekezo na kisha download faili hilo katika kompyuta yako.
Ukishashuka install, hapo unaweza ukawa na uhuru wa kuchagua mambo ya muhimu na kuacha yale yasiyo ya muhimu kwa mfano kutengeneza ‘shortcut’. Unaweza achana nayo yote yasiyo ya muhimu lakini kama unataka WizMouse ifanye kazi ni lazima u’click “Enable mouse wheel for applications without mouse wheel support.” kwa usipofanya hivyo mouse yako inaweza ikafanya kazi kawaida tuu
WINDOWS – shusha
Kumbuka hii ni kwa zile mouse zenye kitairi kwa pale juu tuu
No Comment! Be the first one.