Mtandao wa siku nyingi katika huduma za mtandao wa Yahoo wawakomoa watumiaji wanaotumia huduma za kuzuia matangazo ya mtandao – Ad Blocker.
Katika hatua hiyo iliyopondwa na watumiaji na waandishi mbalimbali duniani mtandao huo uliwazuia watumiaji wa huduma ya barua pepe, yaani Yahoo Mail, kama wanatumia huduma za Ad Blocker.
Biashara nyingi za habari mitandaoni zinategemea kupata mapato kupitia mfumo wa matangazo na hivyo teknolojia za kuzuia matangazo zimekuwa ni adui namba moja kwa mapato ya mitandao mbalimbali.
Mtandao wa Yahoo umeweka teknolojia ya kutambua kama mtumiaji anatumia teknolojia ya Ad Blocker na hivyo kumnyima mtu kutumia huduma ya barua pepe hadi hapo atakaporuhusu matangazo ya mtandao huo kuonekana.
Yahoo waliwezesha zuio ilo kwa masaa kadhaa na inasemekana ilikuwa ni majaribio na wanaangalia kama wanaweza fanya hivyo
Kampuni ya Apple hivi karibuni iliingiza teknolojia ya kuzuia matangazo katika programu endeshaji yake ya iOS kwa ajili ya iPhone na iPad. Apple walilaumiwa na mitandao mbalimbali inayotegemea kupata kipato cha kuendelea kufanya kazi kupitia matangazo yao.
Kwa sasa kuna mitandao mbalimbali katika nchi zilizoendelea walioamua kufanya huduma zao kupatikana kwa watu wanaolipia tuu. Wengi wanaona uamuzi wa Yahoo ni kama wa majaribio tuu na hautadumu, ila unaweza kudumu na ata kuigwa na wengine pia.
No Comment! Be the first one.