fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android simu

Uhakika: Pepsi Wanakuja na Simu Janja Yao, Pepsi Phone P1

Uhakika: Pepsi Wanakuja na Simu Janja Yao, Pepsi Phone P1

Spread the love

Tulishaandika kuhusu habari za chini ya kapeti kuhusu ujio wa simu janja spesheli kutoka kampuni ya vinywaji ya Pepsi. Baadae kampuni hiyo imekubali kuhusu utengenezaji wa simu hizo na huu ndio muonekano wake.

Muonekano wa Pepsi Phone P1

Muonekano wa Pepsi Phone P1

Simu hiyo inayokwenda kwa jina la Pepsi Phone P1 imeshaanza kuuzika kwa mfumo wa kuchangia utengenezaji wake, watu mbalimbali nchini Uchina wanaweza kuchangia gharama za utengenezaji wake na hivyo mara moja kuwa katika orodha ya watu wa kwanza kutumiwa simu hiyo.

SOMA PIA  Anguko la Nokia duniani. Ni kwanini ilianguka? Fahamu zaidi

Sifa ya Pepsi Phone P1

  • Itakuja na uwezo walaini mbili (Micro-SIM na Nano-Sim)
  • Prosesa ya Octa-core MediaTek MT6592 – 1.7GHz
  • RAM GB 2
  • Diski Uhifadhi wa GB 16 na uwezo wa kutumia memori kadi hadi ya ukubwa wa GB 64
  • Inatumia toleo spesheli la Android liitwalo Dido OS, lilotengenezwa kwa kutumia toleo la Android 5.1 lollipop.
  • Bodi la alumini, na kioo cha inchi 5.5 kikiwa na kiwango cha HD – 1080p.
  • Kamera ya nyuma ya Megapixel 13 na ya selfi ya Megapixel 5
  • Betri lisilotoka la kiwango cha mAh 3,000
Pepsi Phone P1

Pepsi Phone P1

Simu hiyo itapatikana katika rangi ya blue, dhahabu na rangi ya fedha (silver). Simu hiyo itauzika kwa bei ya takribani Tsh 400,000/=. Kwa sasa Pepsi wamesema itapatikana Uchina tuu.Wengi wanaona ni kama jaribio na kama simu hiyo itapendwa basi wanaweza kuzitumia katika kujitangaza na promo kwa wapenzi wa vinywaji vyao duniani kote.

Je wewe una maoni gani juu ya hili? Je unadhani utaweza kutumia simu inayobeba jina la kinywaji unachokipenda?

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania