Iphone SE (special edition) ni simu kutoka Apple ambazo wanazitoaga kama toleo maalumu. Mara nyingi toleo hili linaonakana kama simu ndogo (ya nyuma) lakini inakua na vipengele au sifa ambazo ni sawa na simu ya toleo la mbele.
Fununu ni kwamba Apple wana mpango wa kuiachia simu hii mwezi machi mwaka 2020. iPhone hii itakuwa na chip ya A13 ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia katika ufanisi na pia katika uwezo wa betri.

Fununu hizi kama ni za kweli basi kwa mtazamo wangu kutakuwa na tatizo kidogo, ikumbukwe kuwa iPone SE wengi wanazipenda kwa kuwa ni simu yenye umbo dogo, nyemamba na inakua na vipengele/sifa kubwa. Ukiangalia iPhone 8 ni simu kubwa sana na sidhani kama kutakua na tofauti kubwa sana kati ya iPhone 8 na iPhone 8 SE.
iPhone SE ambazo zilitoka mwanzo zilijipatia umaarufu mkubwa sana na wengi walizipenda na kingine kizuri ni kwamba zilikua zinauzwa kwa bei ndogo ukilinganisha na iPhone ambayo ilikua inafananishwa sifa na simu hiyo.
Kwa sasa hakuna taarifa nyingi kuhisiana na fununu hizi kwani hata ukiangalia kampuni bado haijatoa tamko rasmi juu ya jambo hili.