Katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kuna mengi ambayo yanaibuka, kuboreshwa kila leo ili kufanya matumizi mbalimbali ya vifaa vya kidijitali yawe mepesi na kurahisisha ufanisi wa kazi. Ulishawahi kujiuliza diski yenye uwezo wa uhifadhi mkubwa zaidi inaweza kuhimili kiwango gani cha uhifadhi wa data?
Fahamu pia – Tofauti kati ya diski za HDD na za SSD.
Kwa ambao tumesoma masomo ya kompyuta kwa undani kabisa kama taaluma au wale ambao tunapenda kufahamu vitu mbalimbali vinavyohusina na teknolojia tunaweza kufahamu jibu la swali kwenye utangulizi wa makala hii. Lakini hilo si kitu kwani makala hii inalenga kuwaelimisha waliokuwa hawafahamu/kuwakumbusha wale ambao wamesahau.
UTANGULIZI
Mwaka 1956, IBM walileta diski ya uhifadhi data ya kwanza kabisa waliyoiita RAMAC (Random Access of Method Control and Accounting) iliyokuwa na uwezo wa kuhifadhi data za ukubwa wa MB 5 tu. Ukubwa wa memori husika ilikuwa ni kipenyo cha inchi 5024 na ilidumu kwa miaka mitano huku IBM wakiuza nakala 1000.
Mageuzi kwenye ubunifu wa memori
Kadri miaka ilivyozidi kusogea pamoja na teknolojia kukua hivyo hivyo diski uhifadhi zimeendelea kuboreshwa na hadi leo hii tumefikia kwenye memori yenye uwezo wa kuhifadhi wa mpaka Terabyte (TB) ingawa hapo si mwisho.
Utumiaji wa diski hasa za mfumo wa HDD, ulileta mageuzi mengi katika teknolojia za diski kwa ajili ya uhifadhi wa data. Ingawa diski za SSD zimeanza kuwa maarufu kutokana na faida zake hasa hasa kwenye kasi ya usomaji data bado teknolojia yake ipo nyuma linapokuja suala la uwezo mkubwa. Hapa bado ni eneo ambalo diski za aina ya HDD bado zinashika chati.
Fahamu pia – Tofauti kati ya diski za HDD na za SSD.
Kwa sasa diski yenye uwezo mkubwa zaidi wa uhifadhi data ni ya HDD zinazopatikana za hadi za kiwango cha TB 16 ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Seagate. Mwaka huu, tutegemee Seagate kuanza kuuza HDD zitakazochukua nafasi ya juu zaidi, kwa kipimo cha TB 20.
Soma Pia – Jinsi ya kupata nafasi katika diski iliyojaa.
Nikuulize swali rahisi tuu wewe msomaji wetu unamiliki kifaa cha kidijiti ambacho kina uwezo wa kuhifadhi data za ukubwa gani?
Vyanzo: PC World, Secure Data Blog
No Comment! Be the first one.