Kampuni nguli ya Google kupitia mtandao wake namba moja kwa kufuatiliwa duniani itakua inatoa taarifa zile nyeti kwa wahusika endapo kama taarifa hizo zitatafutwa.
Google insema taarifa hizo nyeti ni kama vile namba ya simu, mahali unapokaa, barua pepe yako n.k hili litaanza kufanyika tangia mwanzoni mwa mwaka 2022.
Kinachofanyika ni kwamba kupitia kipengele cha “results about you” (matokeo kuhusu wewe) ndio kitakuachokuwa kinanonyesha mambo yote ya matafuto ukijumuisha na matafuto hayo.
Kipengele cha “results about you” wewe ndio utakua na mamlaka nacho kwa kiasi kikubwa na utaweza kukiruhusu au kukataza kuonyesha baadhi ya taarifa katika matokeo ya matafuto katika mtandao wa Google.

Hii ni moja kati ya njia za muhimu kabisa ambazo Google imekuja nazo, maana taarifa za watu wengi tena zile nyeti kabisa huwa zinaonekana zikizagaa katika mtandao.
Ili kuwezesha hili itakubidi kwenda kujaza fomu ya maombi >>HAPA<<
Kingine ni kwamba kuna baadhi ya watu wameshaanza kujaribu/kutumia kipengele hichi. Pata picha kipengele hichi kitakavyo wasaidia watu wenye hadhi ya juu na mamlaka makubwa kama vile wanasiana ambao wanapitia mambo mengi kama vile vitisho.
https://twitter.com/searchliaison/status/1575197362590343168
Kingine cha kukumbuka ni kwamba Google inakua haileti tuu taarifa ambazo hujaziruhusu lakini ndani katika mitandao husika kaa ukijua taarifa hizo zitakuwa zinapatikana kama kawaida.
Kingine kizuri kuhusiana na kipengele hiki ni kwamba kikianza kutumika na watu wote duniani ni kwamba itakua ni rahisi kujilinda na taarifa zako kwa kufuata hatua chache sana.
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Google >>HAPA<<
ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je umekipokeaje kipengele hiki? Je uko tayari kaunza kukitumia moja kwa moja?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.