Ndio kupitia Google.Com unaweza ukacheza michezo mingi tuu, hii watu wengi hawajui huku wachache wakiambulia ule mchezo (game) wakati hakuna intanet katika kivinjari cha chrome pekee.
Kwa haraka haraka nakuletea michezo 6 ambayo utaweza icheza ndani ya mtandao wa matafuto yaani Google.
Michezo hii ina majina kama ifuatavyo
Google Snake
Hili ni moja ya michezo (game) maarufu sana na huwa vifaa vingi vya kielektronic vinakuja nayo. Mchezo huu huwa unakuja katika vifaa ambavyo hata sio vya kisasa zaidi
Kama kawaida hakikisha nyoka anakula vitu anavyoletewa ili asigonge kuta au kujigusa mwenyewe akiongezeka urefu
Ili Kucheza Mchezo Huu Ingia >>>HAPA au hata >>HAPA
Google Pac-Man
Hata Pac-man ni moja ya michezo maarufu sana na ni ya zamani sana ukilinganisha na michezo mingi tuu.
Kianachofanyika hapa ni kwamba utamchezesha Pac-man kutembea katika maeneo mbali mbali huku akiwa anakula matunda huku akiwakwepa majini — kazi ndogo sio?
Ili Kucheza Mchezo Huu Ingia >>>HAPA
Google Minesweeper
Hii haina tofauti kubwa sana na mchezo wa sodoku, utofauti wake ni kwamba hii ina mabomu. Kinachotakiwa kufanyika hapa ni kuhakikisha kuwa unaziba viboksi vilivyo wazi bila kukutana na bomu…ukikutana nalo mchezo unaishia hapo
Ili Kucheza Mchezo Huu Ingia >>>HAPA
Google Tic-Tac-Toe
Kwa wale wapenzi wa karata hii itawafaa zaidi, mchezo huu na wenyewe sio mpya kwa watu ulikuwepo toka zamani.
Ili Kucheza Mchezo Huu Ingia >>>HAPA
Google Tic-Tac-Toe
Huu ni ule mchezo maarufu kabisa wa kutumia X na O ili kujaza viboksi vilivyo wazi, atakaepatia kujaza viboksi hivyo vitatu kwa mfuatano ndio mshindi
Ili Kucheza Mchezo Huu Ingia >>>HAPA
Google Memory Game
Mchezo huu unahushisha sana kumbukumbu ya sauti, hapa kuna viumbe vinatoa sauti kwa mpangilio husika na wewe itabidi kuzirudia sauti hizo kwa mpangilio huo huo.
Ili Kucheza Mchezo Huu Ingia >>>HAPA
Dino Run (Chrome)
Pengine huu ndio unaweza ukawa ndio mchezo wa Google ambao ni maarufu zaidi na wengi wanakutana nao pale wanapotumia google alaf ghafla mtandao wa intanet ukaleta shida.
Hapa kunakua na kiumba kinachokimbia huku kinakwepa vikwazo fulani mfano kwa kuruka ili kuendelea na safari.
Ili Kucheza Mchezo Huu Ingia >>>HAPA ni lazima uwe na kivinjari (browser) cha Chrome
Leo nimekulee hii ambayo ni michezo michache tuu ambayo unaweza ukaifurahia ndani ya mtandao wa Google.
Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je ni mingapi ulikua unaifahamu au umeshawahi kuicheza, ningependa kusikia kutoka kwako
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.