Gmail ndio mtoaji wa huduma ya barua pepe ambae ni maarufu na anatumika Zaidi kwa watu mbalimbali.
Mara kwa mara huduma hii ya Gmail imekua ikilete maboresho na vipengele kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa inaendana sambamba na matakwa ya watumiaji wake.
Inafahamika kwamba lugha yake ambayo ilikua inatumika kwa miaka kadhaa ni ile ya mfumo wa HTML lakini hili linaenda kubadilika mpaka kufikia mwaka 2024
Kwa sasa wewe ndio una uamuzi kwamba utumia mfumo huu wa zamani (HTML) au utumia mfumo mpya wa Gmail.
HTML ni nini? Pengine hili ndio swali lako kubwa mpaka sasa…
HTML ni mfumo wa lugha ya kawaida ya mtandaoni ambao unatumika katika kuhakikisha kwamba maneno yananekana, rangi zinatokea katika mtandao na muundo mzima wa maneno hayo.
Kirefu cha HTML ni Hyper Text Markup Language nah ii imekua ikitumiwa katika huduma ya Gmail kwa kipindi cha muda mrefu…swali bado linabakia kwanini wanataka kauchana nayo?
Wanachotaka Gmail ni kuhamia katika mababiliko mazuri Zaidi au tunaweza sema ni ya kisasa Zaidi hivyo teknolojia hii itabidi waiache nyuma.
Kwa haraka haraka ni kwamba mabadiliko mapya yatakua hayaendani kabisa namfumo huo wa HTML hivyo basi haina budi kwao.
Mfumo wa HTML ambao ulikua/unatumika kwa Gmail ulikua na faida sana maana ulikua unafanya watu kuweza kutumia huduma hiyo hata katika maeneo ambayo hayana intaneti ya kutosha.
Hata kwa vifaa ambavyo vilikua vinatumia 2G na 3G bado vilikua vinaweza kutumia huduma hii bila ya changamoto yoyote.
Ningependa kusikia kutoka kwakom niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni kuachana kabisa na mfumo na kuhamia katika mfumo mpya.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.