TikTok ni mtandao wa kijamii ambao una video nyingi sana, mtandao huu pia ni moja kati ya mitandao ya kijamii inayojihusisha na maswala ya video ambayo ni maarufu sana.
Licha ya mtandao huwa kuwa unafanya vizuri sana kama mtandao wa kijamii lakini kuna baadhi ya muda hili linatokea kama vile kufuta nyimbo ndani ya mtandao huo.

TikTok wametoa taarifa yao ya uwazi ya miezi mitatu, na ndani ya taarifa hiyo wameweka wazi kuwa wamefuta video hizo milioni 113.
Hapa cha kushangaza ni kwamba ndani ya miezi mitati namba hiyo ya video zilizofutwa ni asilimia moja tuu ya video zilizopandishwa katika mtandao huo ndani ya miezi hiyo mitatu tuu.

Unaweza ukawa unajiuliza ni kwanini mtandao huo umeamua kufuta video hizo, lakini kwa haraka haraka ni ukiukwaji wa sera ya faragha na mambo mengine ya kiulinzi na usalama.
Mambo mengine ambayo yamesababisha video hizo kufutwa ni kama vile shughuli za kiuhalifu, picha/video za ngono au unayanyasaji wa aina hiyo na hata biashara haramu na sababu zingine ndogo ndogo.
Kingine ni kwamba kwa sasa imeonekana dhahiri kuwa idadi ya video ambazo zimefutwa imezidi ukilinganisha na huko mwanzo, pengine sababu inaweza ikawa ni kwamba mtandao unakua, watu wanaongezeka hivyo maudhui yanakuwa ni mengi.
Video hizi zinafutwa moja kwa moja na mfumo maalam wa mtandao huo ambao una kazi maalum ya kufanya hivyo.
Ni wazi kabisa licha ya mtandao huu kupigwa vita vikali na baadhi ya mataifa lakini bado kampuni ilipambana na kuhakikisha kuwa ina jina katika soko la mitandao ya kijamii
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katiaka uwanja wa comment, je unawapa asilimia ngap mtandao wa TikTok kwa kufanya jambo hili?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.