Kwa mwaka huu tunaweza kusema kuwa katika mitandao yote mikubwa ya kijamii, WhatsApp imekuja na vipengele vipya vingi na maboresho mengi sana…… Nimenyoosha mikono!!!
Katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp kuna vipengele vingi sana ambavyo vimeongezeka na vyote ni vikali, na sasa wanakuja na kipengele cha kuweza kuunda link ya kujiunga katika simu za video za makundi.

Mwanzoni ukitaka kumpigia mtu ndani ya mtandao huu ilikua ni lazima uende ukatafute (search) jina lake na uingie katika eneo la mazungumzo na kisha ndio umpigie simu (video au kawaida).
Lakini kuna mitandao mingine kama vile Telegram, iMessage n.k wao huduma ya link wameanza kuitoa mapema tuu na kwa sasa ni zamu ya mtandao wa WhatsApp.

Kwa haraka haraka ni kwamba unaweza ukaanza kutumia kipengele hiki kwa kusambaza link hiyo kwa watu wengine ili wakigusa link hiyo iwapeleke moja kwa moja kwenye simu hiyo ya video.
Kwa sasa mtandao huo unaruhusu simu za makundi ya watu ambao wanafikia 32, ikiwa ni namba kubwa sana kwa video za makundi.
Ukaichana na kuja na kipengele hiki ni kwamba bado kampuni itaendelea kujiboresha zaidi kwa kuleta huduma nzuri na kuongeza baadhi ya vipengele hivyo muda wowote wanaweza wakafanya maboresho mengine.
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Mtandao Huu >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je katika vipengele vyote ambazo WhatsApp wamevitoa hivi karibuni wewe unakipenda sana kipi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.