fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple apps Facebook Intaneti

Facebook vs Apple – Facebook waanza kuomba data za watumiaji wa iPhone

Facebook vs Apple – Facebook waanza kuomba data za watumiaji wa iPhone

Spread the love

Facebook waanza kuomba data za watumiaji wa iPhone baada ya Apple kuanza kuweka ulinzi mpya wa data za watumiaji wa simu za iPhone katika toleo la iOS 14.

Facebook waanza kuomba data za watumiaji wa iPhone

Facebook waanza kuomba data za watumiaji wa iPhone

 

Apple wameleta maboresho katika programu endeshaji ya iOS 14 inayotumika kwenye simu zake na tableti – maboresho yanayopigwa vikali na Facebook. Kupitia maboresho haya kwa sasa programu endeshaji itakuwa inazuia apps zingine kupata taarifa za utumiaji wa apps zingine na tovuti ambazo zinatembelewa na mtumiaji huyo wa simu.

SOMA PIA  Netflix wapandisha bei kwa baadhi ya vifurushi Marekani.

Data hizi huwa muhimu kwa huduma za matangazo ya Facebook kwani ndio data ambazo zinaweza kuwaeleza sifa za mtumiaji wa simu husika – mfano kama una app nyingi za mambo ya mpira na huwa unatembelea zaidi tovuti za mpira basi ni kawaida kujikuta unatumiwa matangazo ya kubeti na mengineyo yanayohusisha vitu kama hivyo.

Apple wamesema wanafanya jitihada kulinda tabia data hizi za watumiaji wake wa simu dhidi ya matumizi mabovu yanayotajirisha makampuni mengine kama vile Facebook.

Kwa sasa watumiaji wa simu hizi watapewa chaguzi la kukubali au kukataa kuzipatia app zingine data muhimu pale watakapozifungua kwa mara ya kwanza. Facebook wanadai uamuzi huu utaathiri biashara nyingi hasa ndogo zinazotegemea kutangaza Facebook ili kupata wateja.

SOMA PIA  Matangazo kwenye WhatsApp Status yapo njiani kuja 2020

Uamuzi wa Apple ni mkubwa sana hasa kwa soko la Marekani ambapo watumiaji wa iPhone ni wengi sana. Suala hili litaathiri biashara ya Facebook kwa kiasi kikubwa. Je Google wanaweza kufanya jambo hilohilo? Ni vigumu kwani nao wanategemea sana biashara ya matangazo.

Vyanzo: CNBC na vyanzo mbalimbali

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania