fbpx

Marekani: Programu ya Antivirus ya Kaspersky Lab marufuku serikalini

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kaspersky Lab marufuku serikalini. Serikali ya Marekani chini ya uongozi wa Rais Trump imepiga marufuku utumiaji wa programu ya antivirus maarufu ya kuzuia virus na mashambulizi ya data kwenye kompyuta ya Kaspersky na huduma zingine zote kutoka kampuni hiyo.

Janga hili limeikuta kampuni ya Kaspersky Lab, watengenezaji wa Antivirus ya Kaspersky, kama muendelezo wa tuhuma zinazofanyiwa uchunguzi juu ya Serikali ya Urusi kushiriki utumiaji wa mtandao katika kushawishi matokeo ya uchaguzi wa Urais uliopita.

Kwa nini janga hili limeikuta Kaspersky?

Kampuni ya Kaspersky makazi yake makuu ni nchini Urusi. Mwanzilishi mkuu wa shirika hilo maarufu duniani, Bwana Eugene Kaspersky ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu ni raia wa Urusi.

Kaspersky Lab ni moja ya kampuni nguli sana katika masuala ya usalama wa data za kikompyuta na sifa hii imeiwezesha kupata mikataba mizuri ya kutoa huduma za kiusalama za kompyuta kwa Serikali nyingi ata nchi za Magharibi kama vile Marekani.

INAYOHUSIANA  Uchina: App kukutaarifu watu wenye madeni ya mikopo benki wakiwa karibu yako

Kwa Marekani huduma zao zimekuwa ni muhimu sana hadi kuwafanya kuwa na ofisi spesheli kwa ajili ya kuhudumia serikali hiyo. Ofisi hii kwa sasa imefungwa baada ya serikali ya Marekani kutoa onyo kwa wizara zake zote.

Kaspersky Lab marufuku serikalini

Ofisi za kitengo cha huduma kwa serikali ya Marekani zikiwa zimefungwa (Kaspersky Government Security Solutions), tawi la Kaspersky Lab North America – ofisi ipo Arlington, Virginia, (Picha na REUTERS/Dustin Volz)

Wizara ya Mambo ya Usalama ya nchini humo (Department of Homeland Security) imezipa taarifa ofisi za serikali nzima ya Marekani ya kwamba wanatakiwa kuzitambua huduma zote za Kaspersky Lab wanazozitumia ndani ya siku 30 na kisha kuhakikisha ndani ya siku 90 huduma hizo zimesitishwa na watamie nyingine mbadala.

INAYOHUSIANA  Marekani: Wadukuzi wafuta barua data za barua pepe zote. #VFEMail

Kaspersky wamefanya nini?

Eugene Kaspersky

Bwana Eugene Kaspersky

Mkurugenzi Mkuu bwana Eugene Kaspersky ameomba kupatiwa hati ya dharula ya kumruhusu kuingia Marekani (Visa) ili aweze kuhojiwa na kamati ya bunge la Marekani inayohusika na uchunguzi juu ya Urusi.

Bwana Kaspersky ameshikilia msimamo wa kwamba kampuni hiyo haijihusishi vyovyote na uvunjifu wowote wa sheria za Marekani na inachukulia shutuma zingine zote kuhusu wao ni kwa sababu tuu kampuni hiyo makazi yake makuu ni Urusi.

Inaonekana ni muhimu sana kwao kujisafisha haraka kwa kamati hiyo kwani wakishindwa watapata hasara nyingi sana kama uamuzi wa serikali ya Marekani ya kutotumia huduma zao utaendelea.

Na vibaya zaidi ni kwamba nchi rafiki za Marekani, hasa hasa zile za Ulaya zinaweza kufuata uamuzi wa Marekani.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.