Kampuni ya Japan ya kutengeneza matairi imesanifu tairi lisilohitaji kuingizwa upepo, na imepata mafanikio katika kuongeza maisha na usalama wa tairi na kupunguza kelele zilizotolewa na tairi wakati gari linapoendeshwa.
Kabla ya hapo, makampuni mengine yaliwahi kusaini matairi ya aina hiyo, lakini hayatumiwi kwa wingi kutokana na tatizo la kelele.
Kampuni hiyo inafahamisha kwamba tairi jipya limepewa jina la “No Air”, ambalo litatumiwa kwenye gari la kawaida.

Tairi hili lina kipenyo cha sentimita 53 na upana wa sentimita 14. Sehemu ya nje ya tairi inatengenezwa na mpira, na ndani inatengenezwa na rasilimali za mseto zinazoimarishwa kwa nyuzi za Carbon.
Ndani ya tairi hili pia kuna njiti 100 za utomvu, ambazo zinasaidia kupunguza shinikizo la tairi na kelele zinazotolewa na tairi.
Likilinganishwa na tairi la kawaida linalohitaji kuingizwa hewa, tairi jipya lina maisha marefu, linapozunguka linakabiliwa na vizuizi vichache, na linaweza kusimamishwa ndani ya muda mfupi wakati dereva anapofunga breki.

Kampuni hiyo inasema tairi hili bado lina dosari chache na itaendelea kuliboresha.
Utafiti wa kutengeneza matairi ya namna hiyo yalianza tangu mwaka 2012 ambapo kadri ya masiku yanavyosonga mbele yamekuwa yakiboreshwa. Kwa sasa matairi hayo yanafanyiwa majaribi kwa magari maalum ili kukagua udhaifu na kuuboresha kabla ya kuanza kutumika katika magari ya kawaida.