fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

simu Uchambuzi

Alpha One: Simu janja ya bei ghali kutoka familia ya Lamborghini

Alpha One: Simu janja ya bei ghali kutoka familia ya Lamborghini

tecno

Simu janja ya Alpha One si ya simu kwa ajili ya kila mtu. Ni simu ghali na hivyo basi wachache sana wataweza kufanya uamuzi wa kuinunua.

Alpha one lamborghini

Simu ya Alpha One, Tonino Lamborghini

Jina la Lamborghini ni maarufu sana kwa kampuni ya utengenezaji magari ya nchini Italia, Automobili Lamborghini, ila simu hii inatengenezwa na kampuni nyingine nguli ya nchini Italia inayojihusisha na bidhaa mbalimbali za ubora wa hali ya juu na ambazo ni za bei ya juu pia – Tonino Lamborghini.

Muanzilishi wa kampuni ya Tonino Lamborghini naye anatokea kwenye familia ileile maarufu inayomiliki kampuni ya utengenezaji magari ya Automobili Lamborghini.

tecno

torino lamborghini

Kampuni ya Tonino Lamborghini inajihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama vile saa, miwani, samani, n.k

Alpha One ni simu janja ya kipekee na yenye mvuto – ila si simu ya kila mtu; ni ya watu wachache na hivyo ni ya bei ghali.

Uchambuzi wa sifa za simu janja-Alpha One.

Alpha One imezinduliwa mwezi Agosti mwaka 2017 ambayo kwa bei yake inaweza ikakushangaza na kukuacha mdomo wazi, cha kujiuliza ni kwanini simu rununu Alpha One kuwa ghali?

Prosesa: Hapa simu hiyo inatumia prosesa ambayo ni maarufu sana kwenye simu za Android, nazungumzia Snapdragon 820 SoC ambayo ina miaka miwili tu tangu kutengenezwa.

>Programu endeshi/Betri: Alpha One inatumia mfumo wa Android 7.0 na betri yake ikiwa na nguvu kiasi cha 3250mAh (betri yake haitoki). Betri yake ina teknolojia ya kujaa chaji haraka yaani QuickCharge 3.0.

>Kioo (Display)/Ukubwa: Kioo chake kina ukubwa wa inchi 5.5 ambacho ni kioo cha mguso na ubora wake ukiwa 1440*2560 pixels. Alpha One ukubwa wake ni 152.00 x 77.00 x 8.00 (urefu*upana*wembamba)

Alpha One inatumia sim card mbili zinzokubali 3G/4G LTE na haitumii teknolojia ya USB OTG ila ina Bluetooth/WI-FI.

Diski ujazo/RAM: Kivutio cha watu wengi kwenye simu janja ni katika kipengele hiki na Alpha One ina ujazo wa ndani wa 64GB na ikiwa na uwezo wa kukubali ujazo wa ziada (micro SD card) wa mpaka 128GB. RAM yake ni ya ukubwa wa 4GB (kwa hakika simu hii ina kasi-kukwamakwama unapoitumia itakuwa ngumu).

>Kamera/Rangi: Kamera yake ya nyuma ina 20MP pamoja na kuwa na uwezo wa kurekodi picha za mnato zenye ubora wa 4K. Kamra yake ya mbele ina 8MP. Alpha One ipo ya rangi moja tu (nyeusi).

>Usalama/Spika: Kama ilivyo simu rununu za siku hizi Alpha One nayo ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole kuifanya simu yako kuwa salama zaidi. Alpha One ina spika mbili za mbele zenye kutoa sauti yenye ubora.

Sifa ya kipekee kwenye simu Alpha One ni kwamba mfuniko wake wa nyuma umetengenezwa kwa ngozi iliyoshonwa kwa mkono.

Bei yake si ya kubeza kabisa, ni $2,450 (Tsh. 5,500,250). Je, unaizungumziaje simu janja kutoka Lamborghini?

Vyanzo: AndrewSoft, Gadgets 360.

SOMA PIA  Bidhaa za Apple zitakazotoka Septemba-Oktoba 2020
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania