Jinsi Ya Kutengeneza Ringtone Katika iPhone!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kwa watumiaji wa iPhone! kama umechoka sikia Ringtone za iPhone ambazo zilikuja simu awali. Ni muda wako wa kubadilisha hilo. Kama unataka kuweka Ringtine za chaguo lako basi hapa ndio mahali pake.

Kwenye kutengeneza Ringtone ni tatizo kwa watumaiji wengi wa simu za Apple kwa sababu njia haipo waziwazi kama katika simu zingine kama za Android.

  • 1. Fungua iTunes na nenda katika miziki yako kutumia kompyuta yako

music

  • 2. ‘Right Click’ Mziki unaoutaka uwe Ringtone yako  na ‘click’ neno ‘Get Info’

getinfo

  • 3. Kitatokea kiboksi chenye maelezo mengi kuhusu hiyo nyimbo. Chagua ‘options’  kisha chagua sehemu ya kuanza na kumalizika kwa ringtone yako. Unaweza chagua sehemu yoyote katika mziki huo iwe ni ya kuanzia lakini mda wa kuanza na kumaliza usizidi sekunde 30. Bofya Ok ukisha  maliza
INAYOHUSIANA  Utumiaji wa Apps za Mitandao ya Kijamii washuka Duniani kote

start_stop

  • 4. ‘Right Click’ katika nyimbo ile ile tena na chagua “Create AAC Version”

kutengeneza mfumo wa Acc unawezesha mafaili kuwa na ujazo mdogo bila ya kupoteza ubora wake. Sasa utaona file jipya katika miziki yako ndani ya iTunes likiwa na jina sawa na lile la mziki uliouchagua. Unaweza kutautisha kwa kuangalia dakika tuu hii nyimbo ya pili itakua ina dakika 0:30 tuu.

INAYOHUSIANA  BlackBerry Wajiunga Na Samsung Katika Kutengeneza Tablet Ya Ulinzi/Usalama Wa Hali Ya Juu!

AAC-version

  • 5.  ‘Right Click’ katika Mziki mpya ulioutengeneza unaoishia sekunde 30 kisha chagua “Show in Windows explorer”
  • 6.  Inabidi ubadilishe jina kutoka mfumo wa .m4a kwenda katika mfumo wa .m4r.  Hii inahitajika kwa kua iTunes inachukulia mfumo wa .m4a kama nyimbo za kawaida (Music) na mfumo wa .m4r  kama mfumo wa ‘Tones’

rename

  • 7. ‘Right Click’ hilo file na kisha ‘open in iTunes’

Ushamaliza kutengeneza Ringtone ya chaguo lako. Na sio lazima iwe nyimbo moja unaweza tengeneza nyimbo nyingi kwa mfumo huu na zote zitakua katika sehemu ya ringtone kwenye simu yako ni wewe tuu kuchagua mojawapo. Unaweza angalia nyimbo ulizozitengeneza zitakua sehemu ya ‘Tones’ katika ‘iTunes’

INAYOHUSIANA  Adidas yatengeneza app yao kwa ajili ya kufanya manunuzi ya bidhaa zao mbalimbali

tones

Jinsi Ya Kuweka Rigntone Katika Iphone Yako

Hii ni rahisi sana ni kama unavyokua una ‘Sync’ iphone yako kawaida tuu.  chomeka USB kwenye simu yako na kompyuta fungua itunes nenda katika iPhone yako. Ukibofya sehemu ya tones utaona zimeongezeka bonyeza ‘Sync’.

Ringtone yako mpya itatokea ukienda katika Settings>Sounds>Ringtone kwenye simu yako. Natumai umeweza tengeneza Ringtone yako mwenyewe mpaka sasa. Msomaji wetu tafadhali Tembelea na kurasa zetu zingine za Twitter, Facebook Na Instagram

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply