Mara baada ya kununuliwa na Facebook, App ya kutuma na kupokea meseji ya whatsApp inajikita katika harakati za kuongezea kupiga na kupokea simu katika App hiyo. Mwanzilishi na mtendaji mkuu wa WhatsApp, Jan Koum, alitangaza kuwa
kampuni jipya la facebook liko mzigoni kuwezesha WhatsApp kupiga na kupokea simu bure, unacho hitaji ni internet tuu. lakini huduma hii itaanza kwanza katika simu za Android na iPhone na baada yatatoka matoleo ya Blackberry na Windows phone.
“Tunaongeza huduma za kupiga na kupokea sauti katika WhatsApp ili watu wawe karibu na wale wawapendao bila kujali wapo mahali gani duniani” alisema bwana Koum katika mkutano wa simu duniani uliofanyika Barcelona
Pia bwana Koum Alisema kuwa amekulia Urusi, “Tulikua na simu lakini majirani wetu wengi hawakua nayo. Hivyo ilikuwa na njia ya mawasiliano ambayo ilikua unatumiwa na kila mtu katika Fleti tulilokua tukiishi. Watu waligonga mlango ili kupigia simu watu mbali mbali katika familia zao ambao walikua nje ya nchi”

Koum alielezea kuwa hii ni stepu nyingine katika mageuzi ya huduma ya WhatsApp. ikiwa inaendeleza lengo lake lile lile la kuwaunganisha watu duniani kote. Pia Kampuni imetumia kasi na ubora wa hali ya juu kutoka katika meseji mpaka sauti na kusema WhatsApp ina huduma nzuri ya sauti.
Hili likiwa tayari basi whatsApp itakua juu ya Skype na juu zaidi ya Viber kwa sababu meseji na kupiga na kupokea simu kutakua kunafanyika kwa haraka zaidi tofauti na App pinzani.
Fununu zingine zinasema kuwa huduma ya Sauti (Free Calls) kutoka WhatsApp itaanza kuwa kama ile ya meseji (mwaka 1 wa kwanza bure na kisha kulipia kila mwaka). Nadhani hilo halina tatizo kama umeweza kutumia WhatsApp upande wa meseji hata huku utaweza pia.
Watumiaji na wapenzi wa WhatsApp kaeni mkao wa kula Toleo jipya liko mbioni kuwafikia katika simu zenu. Msomaji wetu tafadhali Tembelea na kurasa zetu zingine za Twitter, Facebook Na Instagram
No Comment! Be the first one.