fbpx
Apple, apps

iTunes Kutokufa Kabisa Katika Windows!

itunes-kutobadilika-katika-windows
Sambaza

iTunes inamilikiwa na Apple na moja katika ya programu ambazo zinaunganisha vifaa vyote kutoka Apple, hivi juzi juzi,  zilitoloewa taarifa kuwa Apple wenyewe wamesema kuwa App waivunja App hiyo katika App zingine tatu.

Kuhusu kufa kwa iTunes soma hapa.

iTunes itavunjwa katika makundi matatu ambayo ni Apple MusicApple TV na app mpya ya Podcast (Je unataka kujifunza Podcast ni nini? – Soma hapa Teknokona/Podcast). Mabadiliko haya ni wazi hayatakuwepo kwenye windows kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni.

INAYOHUSIANA  Expiry Date? - Apple: Simu mpya ya iPhone inatakiwa kutumika kwa miaka 3
Muonekano Wa iTunes, Ule Wa KAwaida Kabisa Ambao Umezoeleka
Muonekano Wa iTunes, Ule Wa Kawaida Kabisa Ambao Umezoeleka

Apple wamesisitiza kuwa Software yao hiyo itabakia kama ilivyo katika Windows kwani haitavunjwa katika makundi matatu. Kingine ni kwamba kampuni haijasema ni njia gani ambazo itazitumia kuaendesha programu hiyo lakini huduma kwa wateja itawepo

Apple pia hawajatoa taarifa kuhusina na maboresho katika Windows, pia hawajaongelea hata kama kutakuwa na masasisho (updates). Kumbuka pia katika Mac zote kutakuwa na muonekano mpya wa App hii katika makundi matatu… lakini katika windows hakuna uhakika kama kutakuwa na mabadiliko.

INAYOHUSIANA  Instagram yaleta uwezo wa kufuatilia Hashtag

Ni wazi kuwa katika Windows mambo yatabaki vile vile tuu kwani hakuna vipengele ambavyo vitaongezwa pale. Maswali yamekua ni mengi sana kwa watu, wengi wakihisi sawa App inaweza ikawepo lakini kampuni ikawa kama imeisusa tuu.

Je wewe hili unalionaje? ningependa kusikia kutoka kwako, niaindikie hapo chini sehemu ya comment.!

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona, Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com