fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPhone simu

Ujio wa iPhone Mpya-Watu Waweka Kambi Nje ya Maduka!

Spread the love

Wakati yamebakia masaa machache simu mpya za iPhone 5S and 5C kuingia sokoni hizi ni baadhi ya picha za raia mbalimbali huko London na Manhattan, Marekani waliojitokeza siku kadhaa wakisubiri duka kufunguliwa nao wawe wa kwanza kabisa kununua simu hiyo. 

Je wewe unaweza ukawa na mapenzi ya namna hii ya kuacha shughuli zako na kuweka kambi hadi upate kitu kama hichi? tena si bure 🙂 ?

Noah Green aged 17, from London, sits in his plastic greenhouse

Shabiki wa iPhone akiwa nje ya duka la Apple jijini London

Makazi mengine jijini London nje ya Duka la Apple

Ingawa kuna baridi kali lakini halikuweza kuwazuia watu kulala katika kambi hizo

http://www.o2worldnews.com/wp-content/uploads/2013/09/%D8%B9%D9%8F%D8%B4%D8%A7%D9%82-%D8%A2%D8%A8%D9%84-%D9%8A%D8%A8%D8%AF%D8%A3%D9%88%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%AE%D9%8A%D9%8A%D9%85-%D8%A3%D9%85%D8%A7%D9%85-%D9%85%D8%AA%D8%AC%D8%B1%D9%87%D8%A7-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%86%D8%AA%D8%B8%D8%A7%D8%B1-%D8%A2%D9%8A%D9%81%D9%88%D9%86-5-%D8%A5%D8%B3.jpg

Na huko nchini Marekani hali ni kama hii

Wakati iPhone 5S na iPhone 5C zinaingia sokoni masaa machache yajayo mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS 7  tayari ushaanza kupatikana kupitia iTunes kwa watu wenye toleo la iPhone 4 na zaidi, iPad 2 na zaidi, iPad Mini na iPod Touch 5.
Ila hatukushauri kuhamia kwenye iOS 7 kwa sasa, kwani kuna malamiko ya apps nyingi kutofanya vizuri baada ya kuhamia(upgrade) iOS 7. Na utakapoamua kuhamia programu hii hakikisha ume’back up’ vitu vyako kupitia iTunes.


Bei ya chini kabisa ya iPhone 5S inatauzwa takribani Tsh 1,046,837/= wakati iPhone 5C itakuwa takribani Tsh 885,537/=.

SOMA PIA  Walemavu wa kusikia na matumizi ya simu Tanzania
Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania