fbpx

Kwaheri iTunes: Apple waiua iTunes na kuja na apps 3 mbadala

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Sasa ni muda wa kusema kwaheri iTunes. iTunes ni moja ya app maharufu kutoka Apple kwa ajili ya kompyuta za Windows na Macs. Ni app ambayo iliwaletea mafanikio makubwa kibiashara.

Baada ya miaka mingi ya kuendelea kutumika bila mabadiliko makubwa ya utendaji wake sasa Apple wametangaza rasmi ya kwamba muda wa app hiyo kufanyiwa mabadiliko umefika – na haitakuwa mabadiliko tuu bali ni kuondolewa kabisa kwa app hiyo maarufu.

kwaheri itunes

Programu ya iTunes ilileta mabadiliko makubwa ya jinsi watu kuweza kununua nyimbo kwa urahisi

Uondokaji wake unaleta app 3 za kujitegemea. Kutakuwa na programu ya Apple Music, Apple TV na app mpya ya Podcast (Je unataka kujifunza Podcast ni nini? – Soma hapa Teknokona/Podcast)

INAYOHUSIANA  Apps na Programu za Google Drive na Google Photos zatenganishwa

Mabadiliko haya yatakuja rasmi kwenye sasisho jipya la programu endeshaji ya Mac OS inayokwenda kwa jina la Catalina ambayo ipo katika hatua za mwisho wa utengenezaji. Tunategemea baada ya hapo matoleo kwa ajili ya kompyuta za Windows yatafuata.

kwaheri itunes

Kwaheri iTunes: Mabadiliko ya logo ya iTunes miaka na miaka

Kwa MacOS watu wataweza kufanya uhifadhi wa data (backup) wa simu za iPhone moja kwa moja kwenye programu ya mafaili ya Finder – kazi ambayo zamani ilikuwa inafanyika kwenye iTunes.

INAYOHUSIANA  Kwa Ufupi: Habari Mseto za Wiki!

Je umekuwa mtumiaji wa app ya iTunes? Una mtazamo gani na mabadiliko haya yanayokuja?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.