fbpx

UberEats Kuhamia Katika App Ya Uber!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kumbuka tulishawahi andika kuhusu App ya UberEats, App ambao inawawezesha watu kuagiza na kuletewa msosi, kwa sasa kampuni mama yaani Uber imeona ni vyema kabisa kwa App hiyo kuhama na kuingia ndani ya App kuu.

Kuhusu Uber Eats Soma Tena Hapa

Lakini japokua kutakuwa na mabadiliko hayo (UberEats ndani ya Uber) bado App ya UberEats ambayo inajitegemea itakuwepo kama kawaida. Japokuwa katika App mabadailiko ni bado hayajaanza  kuonekana katika baadhi ya nchi, lakini katika tovuti ya Uber tayari kuna kipengele cha Uber Eats.

INAYOHUSIANA  Skype Kutengenezwa Upya Kuwa Kama Snapchat Kwa Microsoft!

Kampuni imesema imefanya hivi makusudi kabisa katika kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata huduma bora kabisa ambayo wataifurahia. Kingine kikubwa ni kamba kampuni ina imani kubwa kuwa kwa kuziweka huduma hizo mbili zote pamoja basi kampuni itaweza kuaongeza matumizi ya kila huduma kutoka kwa wateja.

UberEats Ndani Ya App Ya Uber

UberEats Ndani Ya App Ya Uber

Kingine ni kwamba kuna baadhi ya sehemu huduma hii inaweza ikawa haijafika kwani ndio kwanza ipo katika hatua za mwanzo na mara nyingi kama inavyojulikana inaweza ikawa ndio wakati wa majaribio.

INAYOHUSIANA  Line yajitosa kwenye sarafu zisizoshikika

Mara ya kwanza Uber walikua wanaona kama kuagiza chakula na kuagiza usafiri ni vitu viwili ambavyo haviendani lakini sasa wamebadilisha mawazo yao na kwenda kinyume.

Ikumbuke pia kuwa App ya Uber ni App namba moja duniani katika maswala ya usafiri,hivyo ni wazi kabisa kuwa jambo hili linaweza kwa kiasi kikubwa kuinua zaidi biashara hizo mbili.

Niandikie hapo chini sehemu ya maoni, wewe hili unalichukiliaje? je ni kweli Uber na UberEats itaongezeka katika matumizi.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Na Wewe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.