Samsung kwa mara ya kwanza walipata pigo kubwa sana kuputua simu zao za kujikunja zinazojulikana kama Samsung Fold. Hali ambayo ilipelekea mpaka simu hizo kutolewa sokoni na kurudishwa kwa ajili ya marekebisho.
Sasa kumekuwa na sintofahamu kwamba simu hizo zitarudi lini sokoni na kitu kikubwa kilicho kuwa kinasumbua ni kwamba katika simu hiyo kioo chake kilikuwa kinavunjika bila ya sababu kubwa ya msingi. soma zaidi hapa!
Kizuri cha simu hii ni kwamba ni moja ya simu janja za kisasa zinazokuja na teknolojia ya kujikunja kioo (na kupatikana vioo viwili). Ni simu ambayo wengi walikuwa wanaisubiria kwa hamu kwamba italeta mapinduzi makubwa sana katika simu janja.
Mwezi huu umejulikana baada ya mkuu wa Samsung kunukuliwa akisema kuwa mwezi wa 7 mwaka huu (2019) kuna uwezekano mkubwa sana simu hiyo ikaruidi sokoni.
Kingine ni kwamba kuna ripota (mwandishi wa habari) ambae nae amekiri kuwa kasikia taarifa hiyo hiyo kuhusina na tarehe ya kurejesha sokoni simu hizo
I heard from a source that the Galaxy Fold will launch in July. I heard this a few days ago, but now there is a website quoting a Samsung executive saying they would like to see a July launch, but a press conference before that. https://t.co/eu6ahD40cy
— Max Weinbach (@MaxWinebach) June 7, 2019