Watumiaji wa simu za iPhone 6 (walio pakua iOS mpya) ambao walitengeneza simu zao kupitia mafundi ambao hawajaandikishwa na Apple wamepatwa na hali ya sintofahamu baada ya simu zao kufungiwa baada ya update ya OS hiyo.
Simu hizi ambazo zimegundulika zilitengenezwa na mafundi wasio sajiliwa na kampuni hii zimefungiwa na zinaonesha Error 53 hakuna unachoweza kufanya hata kama utataka kurudi katika OS ya zamani pia hilo hutaweza.
Kiufundi ni kwamba unapofanya update ya software ya iPhone 6 basi inafikia mahali hii OS mpya inaichunguza simu kama kuna kifaa ambacho sio kutoka kwa mafundi wake walio sajiliwa kufanya matengenezo ya simu hizo ambazo zina gharama kubwa.
Mtandao wa the Guardian wa huko Uingereza unaripoti kwamba watumiaji wa simu za iPhone 6 ambao kwa namna moja au nyingine walifanya matengenezo ya simu zao ambayo yalihusisha kubadilisha baadhi ya vifaa na kuwekewa vifaa ambavyo sio vile vilivyothibitishwa basi wamekutana na kadhia hii.
Baada ya ripoti hii kuchapishwa na jarida hilo Apple walitoa statement kusema kwamba wanachukulia usalama wa watumiaji wao kuwa ni kitu muhimu na kwamba Error 53 imewekwa ili kuhakikisha kwamba vifaa vya home button vinaendana na vifaa vingine ndani ya simu yako na pia ni vile ambavyo ni halali.
Taarifa kutoka Apple inawataka watumiaji ambao wanakumbana na kadhia hiyo kuwasiliana na huduma kwa wateja wa Apple kwa msaada zaidi.
Tayari kuna makundi yanafikiria kuishtaki Apple
Fikiria umenunua gari kutoka Toyota na ikasumbua ukaenda kwa fundi wako wa bei rahisi na akarekebisha labda kwa kubadili kifaa kama vile alternator. Baada ya muda Toyota wakigundua hilo wazuie gari lako kufanya kazi kabisa kisa tuu ujatumia huduma zao ambazo huwa ni za bei ya juu….hili suala halileti maana. Na inaonekana kama mashitaki hayo yakifika mahakamani basi kuna uwezekano mkubwa Apple watakutwa na hatia kisheria.
Error 53 itakuwa ni sababu nyingine kwa watumiaji wa kipato cha chini huku Afrika mashariki kuzikimbia simu hizi kwani pindi zinapo pata matatizo ni gharama sana kutengeneza ukilinganisha na simu za Android ambazo mafundi wake wapo wengi sana mitaani.
No Comment! Be the first one.