Ile kero ambayo ilikuwa ikiwasumbua wengi wakati wa kuperuzi kwenye kivinjari cha Safari (vifaa vinavyotumia iOS) ipo mbioni kuisha mara tu toleo jipya la iOS 11 litakapotoka.
Kwa kitendo cha Apple kuamua kufungia yale matangazo ambayo hayana hata mpangilio maalum wa kutokea ni dhahiri shairi linakera kupita kiasi; wakati unaperuzi tovuti/ukurasa fulani ghafla unashanga tangazo linatokea mbele ya ukurasa ambao upo.
Ni jambo lenye kufedhehesha na linapoteza umakini wa kile ambacho ulikuwa unakisoma au kukifuatilia kwenye tovuti husika.
iOS 11 toleo jipya ambayo ipo kwenye simu za Apple zilizozinduliwa itakuwa ni jambo la furaha kwa yeyote yule ambaye atanunua moja kati ya simu hizo zilizozinduliwa na kufurahia mengi tu yaliyoboreshwa na mambo mengine mapya kwenye programu endeshi ya iOS 11, kujua mengi zaidi kuhusu iOS 11 BOFYA HAPA!
Mbinu itakayotumika kuzuia matangazo kwenye kivinjari cha Safari 11.
Katika toleo jipya la iOS 11 Apple wametumia teknolojia inayofahamika kama “intelligent tracking prevention system” kwa lugha ya kimombo. Kwa maana ya kwamba teknolojia hiyo itakuwa na uwezo wa kuzuia kabisa yale matangazo ambayo mtumiaji hawezi kuyazuia (first party) na yale ambayo mtu anaweza kuyazuia kwenye kivinjari yanafahamika kama third party.

Kampuni zinazojihusisha na biashara ya matangazo kwenye mitandao tayari zimeshaiandikia Apple kuwaomba wafikirie mara mbili kuhusu uamuzi huo ila Apple wamesema matangazo hayo yamekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa iOS.
Toleo jipya la iOS 11 litaanza kupatikana Septemba 25 kwa watumiaji wa iOS kwa kufanya masasisho kuanzia hiyo tarehe ila cha kuzingatia ni kuhakikisha intaneti unayotumia ina kasi, isije ikakwama wakati wa kufanya masasisho kwenye iPhone/iPad au kompyuta.
Vyanzo: TechCrunch, The guardian