Licha ya kwamba kila mtu anaweza akawa na mtazamo wake juu hili. Tukisema turopoke tuu hatutapaja jibu kamwe, lazima tuweke misingi ambayo itatuwezesha kujua nani ni zaidi kuliko mwenzake.
Sawa kampuni zote zinamilikiwa na mtu mmoja lakini kumbuka makampuni haya mawili yanajitegemea kabisaa! Na leo tutakujuza nani zaidi.
Ili kumjua nani mkali tutakujibu kwa kuangalia
1. Hadhi kwa mtumiaji
2. Uwezo wake wa kukufanya Mraibu (Addict)
3. Je ni njia nzuri ya kuweza kuwasiliana na jamii?

Moja kwa moja tuanze na kipengele cha kwanza
1. Hadhi kwa mtumiaji
Hapa tunaangali ni mtandao gani ambao unakupa hadhi kubwa kuliko mingine katika hii miwili. Hapa bila kupoteza muda jibu ni mtandao wa Facebook. Kumbuka ukiwa ndani ya mtandao huo unaweza ukafanya mambo mengi sana kama vili kijiunga katika makundi (group) kadhaa.
Makundi haya yanaweza yakawa na msaada mkubwa sana kwako, kama vile ukiwa na maswali, taarifa mbalimbali, kukusaidi katika kazi Fulani, kukutunisha na watu ambao unashabihiana nao katika kazi yako n.k.
Kwa kutumia mtandao wa Facebook pia ni njia nzuri ya kujua ni vitu gani vinatokea katika jiji lako kwa kupitia kipengele cha matukio (Events). Kwa hili Facebook imeishinda Instagram kwa sababu kwa vipengele hizi, bado haijaifikia Facebook karibu
2. Uwezo wake wa kukufanya Mraibu (Addict)/ Unakuburudisha kiasi gani?
Ili mtandao Fulani ukufanye uweze kuufungua mara kwa mara ili mradi kutupia jicho ndani na kuona kitu kilicho’postiwa na marafiki zako lazima uwe unakupa burudani ya aina yake. Kumbuka burudani ya aina yake inaweza ikakufanya kuwa mraibu wa mtandao huo… Sasa hapa tunaangali ni mtandao gani ambao unaweza ukakufanya kutamani kuufungua mara kwa mara ili kuona nini kiko ndani?

Hapa nadhani umeshajua ni mtandao upo… bado? Haya kama bado basi jibu ni mtandao wa Instagram. Uwezo wake wa kukuwezesha kuangalia picha za marafiki zako mara kwa mara unaweza ukakufanya kurudi rudi kila mara katika mtandao huo ili kuona nini tena wametuma.
Sawa unaweza ukasema kuwa Facebook nao wana huduma sawa ya kutuma picha lakini ukweli ni kwamba katika Instagram picha mambo mengi unayoyona ni kwamba ume amua kuyaona (follow) wewe mwenyewe tofauti na Facebook ambako unaweza ukaona hadi picha za marafiki wa marafiki zako kupita kipengele cha ‘Tag’. Vitu ambazo unavifuatilia katika mtandao wa Instagram kwa watu tofauti tofauti vinaweza vikakurudisha mara kwa mara katika mtandao huo.
3. Je ni njia nzuri ya kuweza kuwasiliana na jamii?
Nafikiri kazi kubwa ya mitandao ya kijamii ni kuwa na uwezo wa hali ya juu wa kukuwezesha wewe kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki na hata ku ‘share’ nao nyakati tofauti tofauti. Sasa kwa kuangalia hili ni mtandao gani mzuri ambao unaweza liwezesha hili kati yah ii miwili

Kwa mara nyingine facebook inaonekana ina uwezo mkuwa juu ya hili. Kumbuka ndani ya mtandao huo mtu unaweza ukaandika post, kuwatakia (heri za siku ya kuzaliwa, sikukuu, mwaka mpya n.k), ku comment katika picha za marafiki zako, kutuma meseji baina yenu wawili tuu au ukaamua kutuma meseji na kuongea na kundi. Pia kumbuka unaweza uka’share’ picha au tukio la zamani kwa kutumia kipengele cha ‘Memories’ katika Facebook.
Instagram kwa upande mwingine imejikiita tuu katika kuangalia picha/video za marafiki zako na ku’comment’ juu yake. Kuwa na mawasiliano baina ya wawili au kundi. Kwa kuangalia namna ambayo mtu anaweza akawasiliana na jamii yake vizuri basi Facebook ina hadhi kubwa katika kuliwezesha hilo.
Kwa kuyasema hayo nadhani hapo kila kitu kipo wazi juu ya nani anaongoza… labda nikuulize swali, hivi ni mtandao gani ambao unaufungua mara kwa mara na kufanya mambo mengi zaidi, kati ya hiyo miwili?